BoT: Faini 500,000 au kifungo mwaka mmoja ukiharibu noti

November 6, 2026 6:48 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Kwa mujibu wa Kifungu cha 332A cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu (Penal Code), Sura ya 16, Toleo la Marejeo la 2023, mtu yeyote ambaye bila mamlaka, kwa makusudi anaharibu, anararua, anakata au kuharibu kwa namna nyingine noti ya fedha inayotumika kisheria nchini, anatenda kosa la jinai.

Dar es Salaam. Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema mtu atakayepatikana na hatia ya kuharibu noti za Tanzania kwa makusudi anaweza kutozwa faini ya Sh500,000 kwa kila noti au kifungo cha mwaka mmoja jela.

Onyo hilo ambalo ni kwa mujibu wa Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya Tanzania Sura ya 16 linakuja wakati baadhi ya wananchi wamekuwa na mazoea ya kuziharibu noti kwa kuzichora, kuzichana, kuzirusha au kuzimwaga chini.

Shadrack Mapunda, Ofisa wa BoT kutoka Kurugenzi ya Sarafu aliyekuwa akizungumza leo Novemba 6, 2026 wakati wa mafunzo kuhusu usalama na  utunzaji bora wa fedha amesema vitendo hivyo ni vinachangia uchakavu wa noti na kuongeza gharama za kuzalisha fedha mpya.

Mapunda amesema baadhi ya wananchi hawana utamaduni mzuri wa kutunza fedha za Tanzania, huku wengine wakithamini zaidi fedha za kigeni ikiwemo noti za Dola za Marekani kuliko shilingi.

Mapunda amesema baadhi ya wananchi hawana utamaduni mzuri wa kutunza fedha za Tanzania, huku wengine wakithamini zaidi fedha za kigeni ikiwemo noti za Dola za Marekani kuliko shilingi. Picha | BoT

Amesema badala ya kuamini kuwa kuchana noti au kuweka vitu ndani yake kunaweza kuleta bahati au kuzuia imani za kishirikina, wananchi wanapaswa kutumia njia mbadala za malipo, ikiwemo mifumo ya kidijitali.

“Ukiona kuchua cash ni ‘chuma ulete’, weka lipa namba. Kwani kuna chumaulete kwenye lipa namba? Kuna njia nyingi za kidijitali za kufanya malipo,” amesema Mapunda.

Kwa mujibu wa Kifungu cha 332A cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu (Penal Code), Sura ya 16, Toleo la Marejeo la 2023, mtu yeyote ambaye bila mamlaka, kwa makusudi anaharibu, anararua, anakata au kuharibu kwa namna nyingine noti ya fedha inayotumika kisheria nchini, anatenda kosa la jinai.

Akitiwa hatiani, anaweza kutozwa faini ya Sh500,000 kwa kila noti iliyoharibiwa au, asipolipa faini hiyo, kufungwa jela kwa mwaka mmoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
6 Nov, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
6 Nov, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
BEI YA MAFUTA DAR | Sh10,000 kununua lita 2.44 za petroli, 2.42 za dizeli

BEI YA MAFUTA DAR | Sh10,000 kununua lita 2.44 za petroli, 2.42 za dizeli

Nukta TV

Namna Rais Samia alivyoshiriki kwenye Uchaguzi Mdogo, Jimbo la Chamwino

Namna Rais Samia alivyoshiriki kwenye Uchaguzi Mdogo, Jimbo la Chamwino

Nukta TV

Ndejembi: Wanachamwino wameona kwa macho, mrithi wangu ataendeleza kasi ileile

Ndejembi: Wanachamwino wameona kwa macho, mrithi wangu ataendeleza kasi ileile

Nukta TV