Rais Samia atoa maagizo manne, mji wa Serikali Mtumba

October 30, 2026 5:32 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Awataka watumishi wa umma kuongeza uwajibikaji katika majukumu yao na kusisitiza mifumo ya taasisi kusomana ili kuondoa ulazima wa mwananchi kufuata kila huduma katika mji huo.

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ametoa maagizo manne kwa viongozi na watendaji wa Serikali kuhakikisha Mji wa Serikali Mtumba, unatunzwa na kuendelezwa kwa mpangilio na miundombinu inayokidhi mahitaji ya watumishi na wananchi katika utoaji huduma.

Akizungumza leo Oktoba 30, 2026 katika uzinduzi wa mji huo jijini Dodoma, Rais Samia amewataka viongozi kuhakikisha miundombinu na mazingira ya mji huo inatunzwa, akimtaka Katibu Mkuu Kiongozi kushirikiana na makatibu wakuu kusimamia utunzaji wa maeneo ya kijani na upandaji miti ili kuongeza uoto wa asili jiji hilo.

Rais Samia aliyeambatana na Rais wa Angola, João Lourenço katika uzinduzi, pia ameitaka Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), kushirikiana na Wizara ya Ardhi na taasisi nyingine, kutekeleza mpango mkuu wa jiji la Dodoma wa mwaka 2019-2039 kudhibiti ujenzi holela na uvamizi wa maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya huduma za jamii.

“Itakuwa ni aibu kubwa, tuna mpango mzuri sana wa jiji la Dodoma, alafu tukute kuna uvamizi umetokea bila kuheshimu ‘master plan’ hiyo,” amesisitiza Rais Samia.

Rais Samia, amewataka watumishi wa umma kuongeza uwajibikaji katika kutekeleza majukumu yao na kusisitiza mifumo ya taasisi kusomana ili kuondoa ulazima wa mwananchi kufuata kila huduma katika jiji la Dodoma. Picha | Ikulu Mawasiliano.

Katika agizo lingine, Rais Samia amezitaka wizara zinazohusika kuhakikisha upatikanaji wa uhakika wa huduma za msingi ikiwemo umeme, maji na barabara.

Aidha, ameitaka Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji kushirikiana na sekta binafsi kuweka mikakati ya kuvutia uwekezaji utakaosaidia kukuza maendeleo ya jiji la Dodoma.

Kilele cha safari ya miaka 53 

Licha ya Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kuzindua rasmi Mji wa Serikali Mtumba, ndoto ya kuifanya Dodoma kuwa makao makuu ya nchi ni safari iliyochukua zaidi ya nusu karne, tangu ilipoasisiwa mwaka 1973 chini ya uongozi wa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere. 

Jitihada za kutekeleza azma hiyo ziliendelea katika awamu za marais Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete, hadi mwaka 2016 ambapo Rais wa Awamu ya Tano, Hayati John Pombe Magufuli, alipoamua kuharakisha uhamishaji wa shughuli za Serikali kwenda katika jiji hilo. 

Mji wa Serikali, Mtumba, ulitengwa kwa ajili ya kukusanya wizara, taasisi na ofisi mbalimbali za Serikali katika eneo moja, kwa lengo la kurahisisha uratibu wa shughuli za Serikali na kurahisisha wananchi kupata huduma wanazohitaji bila kulazimika kufuata ofisi katika maeneo tofauti. 

Mji huo uliojengwa kwa takriban Sh700 bilioni za Watanzania, unajumuisha majengo 37 ya ofisi za wizara na taasisi za Serikali, mtandao wa barabara za lami wenye urefu wa kilomita 59.1, vituo 52 vya mabasi pamoja na miundombinu mingine inayowezesha urahisishwaji wa huduma. 

Sambamba na maelekezo yote aliyoyatoa Rais Samia, amewataka watumishi wa umma kuongeza uwajibikaji katika kutekeleza majukumu yao na kusisitiza mifumo ya taasisi kusomana ili kuondoa ulazima wa mwananchi kufuata kila huduma katika jiji la Dodoma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
30 Oct, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
30 Oct, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
30 Oct, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Tanzania na Angola kuunganisha reli na safari za ndege

Tanzania na Angola kuunganisha reli na safari za ndege

Nukta TV

Tanzania kufungua tena ubalozi Angola, Balozi mpya kuteuliwa

Tanzania kufungua tena ubalozi Angola, Balozi mpya kuteuliwa

Nukta TV

Makonda: 28 - 30 Oktoba ni siku za kumshukuru Mungu kwa kuitunza amani ya Tanzania

Makonda: 28 - 30 Oktoba ni siku za kumshukuru Mungu kwa kuitunza amani ya Tanzania

Nukta TV