Mikoa 10 tajiri zaidi Tanzania Bara 2025

October 24, 2026 2:09 pm · Method Allen
Share
Tweet
Copy Link
  • Tangu hata kabla ya kupatikana kwa uhuru Dar es Salaam imekuwa moja kati ya mikoa yenye shughuli nyingi zaidi za kiuchumi ikiwemo biashara zinazochagizwa na uwepo wa vitega uchumi vingi ikiwemo bandari, miundombinu ya usarifishaji na masoko ya kimataifa kama kariakoo.

Dar es Salaam. Mkoa wa Dar es Salaam umeendelea kuonyesha ubabe kiuchumi kwa zaidi ya miaka kumi mfululizo kwa kuwa ndio mkoa wenye pato kubwa zaidi kuliko mikoa yote Tanzania bara, ukurekodi pato la Sh39.8 trilioni kwa mwaka 2025. 

Kwa mujibu wa ripoti ya utendaji wa uchumi wa kanda inayotolewa na Benki Kuu ya Tanzania. Pato hilo la mkoa ambalo ni la juu zaidi kuwahi kurekodiwa tangu mwaka 1973 Dar es Salaam ilipotenganishwa na Pwani ni sawa na asilimia 17 ya pato lote la Taifa la Sh234.1 trilioni lilorekodiwa mwaka 2025.

Kulinganisha na mwaka uliopita, pato la mkoa wa Dar es Salaam liliongezeka kwa asilimia 14.37 kutoka Sh34.8 trilioni iliyorekodiwa mwaka 2024.

Tangu hata kabla ya kupatikana kwa uhuru Dar es Salaam imekuwa moja kati ya mikoa yenye shughuli nyingi zaidi za kiuchumi ikiwemo biashara zinazochagizwa na uwepo wa vitega uchumi vingi ikiwemo bandari, miundombinu ya usarifishaji na masoko ya kimataifa kama kariakoo.

Licha ya kuwa na Ziwa Victoria, jiji la Mwanza ambalo ni maarufu kwa shughuli za uvuvi na uchimbaji madini limeshika nafasi ya pili likirekodi pato la Sh16.7 trilioni sawa na nusu ya pato la mkoa wa Dar es Salaam.

Mkoa wa Mbeya ambao ni kitovu cha shughuli za kilimo cha mpunga na mahindi, umeshika nafasi ya tatu ukirekodi pato la Sh12.9 trilioni. 

Mikoa mingine iliyoingia kwenye sita bora ni Morogoro ambao ni maarufu kwa shughuli za kilimo, ufugaji na utalii ikishika nafasi ya nne kwa kurekodi pato la Sh11.4 trilioni, ukifuatiwa na Arusha ambao ni maarufu kwa shughuli za kiutalii ukirekodi Sh11.1 trilioni.

Tanga ambayo ni maarufu kwa shuguli za kilimo cha biashara ikiwemo katani na chai imeshika nafasi ya sita ikirekodi pato la Sh10.9 trilioni ikifuatiwa na mikoa ya Geita na kilimanjaro iliyorekodi kipato cha Sh10.5 trilioni kila mmoja.

Mkoa wa Tabora  na mara imefunga orodha ya kumi bora ikirekodi kipato cha Sh8.7 trilioni na Sh8.6 trilioni mtawalia.

Mtazamaji hiyo ndiyo mikoa tajiri kuliko mikoa yete Tanzania Bara, katika orodha hiyo chama lako limeshina namba ngapi, tuambie kwenye comment.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
24 Oct, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
24 Oct, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Namna uhaba wa nyani, pofu unavyohatarisha ndoa za Wahadzabe

Namna uhaba wa nyani, pofu unavyohatarisha ndoa za Wahadzabe

Nukta TV

Hii ndio mikoa yenye watu wenye kipato kikubwa zaidi Tanzania

Hii ndio mikoa yenye watu wenye kipato kikubwa zaidi Tanzania

Nukta TV

Uhaba wa maji unavyozitesa jamii za asili, wakiwemo Wahadzabe, Karatu, Tanzania

Uhaba wa maji unavyozitesa jamii za asili, wakiwemo Wahadzabe, Karatu, Tanzania

Nukta TV