TRA yavunja rekodi ya makusanyo miezi 27 mfululizo

October 5, 2026 4:59 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Septemba ndiyo iliyokuwa na makusanyo makubwa zaidi katika robo hiyo, ambapo Sh4.19 trilioni zilikusanywa dhidi ya lengo la Sh3.96 trilioni, sawa na ufanisi wa asilimia 105.71. 

Dar es Salaam . Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imevunja rekodi ya makusanyo katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026/27, baada ya kukusanya Sh10.65 trilioni kati ya Julai na Septemba 2026, ikiwa ni mwezi wa 27 mfululizo wa kuvuka malengo tangu Julai 2024.

Kwa mujibu wa taarifa ya TRA, makusanyo hayo ni sawa na asilimia 107.49 ya lengo la Sh9.91 trilioni, huku yakiongezeka kwa asilimia 18.81 kutoka Sh8.96 trilioni zilizokusanywa katika kipindi kama hicho mwaka wa fedha 2025/26.

Katika miezi hiyo mitatu, TRA ilikusanya Sh3.25 trilioni Julai, Sh3.22 trilioni huku Septemba ikiwa ndiyo mwezi wenye makusanyo makubwa zaidi katika robo hiyo, ambapo Sh4.19 trilioni zilikusanywa dhidi ya lengo la Sh3.96 trilioni, sawa na ufanisi wa asilimia 105.71. 

TRA imesema ongezeko hilo limechangiwa na uboreshaji wa mifumo ya ukusanyaji kodi, huduma kwa walipakodi, mazingira ya biashara na hatua za kudhibiti ukwepaji kodi.

Katika kupanua wigo wa kodi, TRA imesajili walipakodi wapya 447,611 katika robo hiyo, na kufikisha jumla ya walipakodi waliosajiliwa 9,011,783 kutoka 8,564,172 waliokuwepo Juni 2026.

Aidha, mamlaka hiyo ilibaini biashara 18,658 ambazo hazikuwa zimesajiliwa na kusaidia biashara 10,778 kurasimishwa kwa hiari.

Katika kudhibiti ukwepaji kodi, TRA ilikamilisha uchunguzi wa zaidi ya kesi 130, ambapo Sh331.15 bilioni zilibainika na zaidi ya Sh44.74 bilioni kukusanywa.

Pia, doria 1,185 dhidi ya magendo zilifanyika na bidhaa zenye thamani ya Sh12.72 bilioni kukamatwa, huku Sh5.34 bilioni za kodi zikikombolewa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
30 Oct, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
30 Oct, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Tanzania na Angola kuunganisha reli na safari za ndege

Tanzania na Angola kuunganisha reli na safari za ndege

Nukta TV

Tanzania kufungua tena ubalozi Angola, Balozi mpya kuteuliwa

Tanzania kufungua tena ubalozi Angola, Balozi mpya kuteuliwa

Nukta TV

Makonda: 28 - 30 Oktoba ni siku za kumshukuru Mungu kwa kuitunza amani ya Tanzania

Makonda: 28 - 30 Oktoba ni siku za kumshukuru Mungu kwa kuitunza amani ya Tanzania

Nukta TV