Samir Yassine ateuliwa CEO mpya BOA Tanzania

August 14, 2026 3:08 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Yassine anaingia katika nafasi hiyo akiwa na zaidi ya miaka 26 ya uzoefu katika sekta ya benki na huduma za kifedha.

Dar es Salaam. Samir Yassine ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji (CEO) mpya wa benki ya biashara ya Bank of Africa Tanzania (BOA) kuiongoza taasisi hiyo ya kifedha yenye zaidi ya miaka 19 nchini.

Yassine anaingia katika nafasi hiyo akiwa na zaidi ya miaka 26 ya uzoefu katika sekta ya benki na huduma za kifedha akiwa amejikita zaidi katika maeneo ya maendeleo ya biashara pamoja na uongozi wa juu.

Bodi ya Wakurugenzi ya Bank of Africa Tanzania Limited imemteua Yassine katika kipindi ambacho sekta ya benki inakua kwa kasi zaidi nchini huku sehemu kubwa ya benki za biashara zikiripoti faida.  

Uteuzi huo unaashiria mwanzo wa hatua mpya ya ukuaji, ubunifu na ubora katika utoaji wa huduma katika sekta ya fedha tangu benki hiyo ilipoanzishwa mwaka 2007.

Kabla ya kuteuliwa kuwa bosi wa juu wa BOA Tanzania, Yassine alikuwa ni sehemu ya uongozi wa benki hiyo akihudumu kama Naibu Mkurugenzi Mtendaji anayesimamia biashara kwa kipindi cha miaka mitano kabla ya kutangazwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa BOA Uganda mwaka 2024.

Kabla ya kuteuliwa kuwa bosi wa juu wa BOA Tanzania, Yassine alikuwa ni sehemu ya uongozi wa benki hiyo akihudumu kama Naibu Mkurugenzi Mtendaji anayesimamia biashara kwa kipindi cha miaka mitano kabla ya kutangazwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa BOA Uganda mwaka 2024. Picha | New Version

Kabla ya kufanya kazi ndani ya Bank of Africa Group, mtandao wenye benki 18 za kibiashara ndani ya Bara la Afrika na Ulaya, Yassine pia aliwahi kushika nafasi mbalimbali ikiwemo Afisa Uhusiano pamoja na huduma za kifedha kwa biashara (Trade finance) ndani ya benki ya BMCE nchini Morocco.

Uteuzi, kijiti cha kusongesha gurudumu la faida

Hata hivyo, uteuzi wa Yassine unakuja wakati ambao BOA Tanzania inaendelea kuboresha utendaji wake wa kifedha licha ya kuongezeka kwa ushindani mkali sokoni. 

Kwa mujibu wa ripoti rasmi ya fedha ya Bank of Africa Tanzania ya mwaka 2024, mapato ya benki hiyo yaliongezeka kwa asilimia 4.1 hadi Sh61.4 bilioni, kutoka Sh59 bilioni mwaka 2023. 

Aidha, faida baada ya kodi nayo iliongezeka kwa asilimia 18.9 ikikua kutoka Sh11.03 bilioni mwaka 2023 hadi Sh13.12 bilioni mwaka 2024.

Kwa upande wa faida kabla ya kodi, benki ilirekodi Sh20.1 bilioni mwaka 2024, kutoka Sh16.1 bilioni mwaka 2023, sawa na ongezeko la asilimia 24.8 huku ukuaji wa mapato hayo ukichangiwa zaidi na miamala ya fedha za kigeni yaliyoongezeka kwa asilimia 34.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
14 Aug, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
14 Aug, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia awataka wananchi wa Kizimkazi kutunza miundombinu ya maji

Rais Samia awataka wananchi wa Kizimkazi kutunza miundombinu ya maji

Nukta TV

Ni changamoto gani zinawakabili vijana wa kitanzania kwa sasa ?

Ni changamoto gani zinawakabili vijana wa kitanzania kwa sasa ?

Nukta TV

Akili Unde (AI) ni suluhu ya habari za uzushi ?

Akili Unde (AI) ni suluhu ya habari za uzushi ?

Nukta TV