Maisha bila friji: Mbinu tano za asili za kuhifadhi chakula

August 10, 2026 3:08 pm · Method Allen
Share
Tweet
Copy Link
  • Jamii nyingi za Afrika zilikuwa tayari zimebuni njia mbalimbali za uhifadhi wa chakula kwa kwa muda mrefu kuanzia wiki, miezi na hata msimu mzima

Dar es salaam. Historia inaonesha kuwa mababu zetu walihifadhi chakula kwa muda mrefu bila jokofu, wakitumia mbinu za asili zilizotegemea jua, chumvi, moshi na udongo. 

Kwa vizazi vya sasa, uhifadhi huo unaweza kuonekana wa kizamani kutokana na utegemezi mkubwa wa jokofu teknolojia iliyosambaa duniani kuanzia karne ya 20 baada ya ugunduzi wa Fred W. Wolf.

Licha ya matumizi makubwa ya jokofu, FAO inakadiria kuwa takribani asilimia 14 ya chakula hupotea kati ya mavuno na kufika sokoni, huku  ukiwaathiri mamia ya watu ikiwemo waishio Tanzania.

Kutokana na changamoto hiyo, Jiko Point imekusanya mbinu tano za asili zinazoweza kusaidia kuhifadhi chakula bila jokofu na kukifanya kidumu kwa muda mrefu.

Uhifadhi wa kutumia moshi

Kwa mujibu wa ripoti ya utafiti wa uhifadhi wa chakula uliofanywa na Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA) kuhifadhi chakula kwa kutumia moshi (fukuto) huongeza ladha na uezo wa chakula kuhidahiwa kwa muda mrefu.

Jamii nyingi, hasa za maeneo ya karibu na maziwa na bahari, bado zinatumia mbinu hii kuhifadhi samaki na nyama, chakula suala linalowafanya kuwa na akiba ya kutosha ya chakula na kingine kutumika kwa ajili ya biashara.

Njia ya uhifadhi wa chakula kwa kufukizia moshi iliyotumika na jamii ya waafrika kabla ya ujio wa njia za kisasa za uhifadhi wa chakula aina ya nyama, samaki na dagaa
| picha Galactic

Kukausha kwa kutumia mwanga wa jua

Hii ilikuwa moja ya njia maarufu zaidi katika jamii nyingi za Afrika, mazao kama vile Mahindi, mpunga, mihogo, samaki, dagaa, nyama, matunda na mboga zilitandazwa juani hadi kupoteza unyevu.

Mzee Gerard kutoka Kilosa, Morogoro ameiambia Nukta habari kuwa njia ya uhifadhi wa mazao kwa kukausha juani ni njia ambayo bado inatumika hata sasa

“Tumekua tunatumia njia hii siku zote tangu kuzaliwa kwetu, tulikuta mababu wanaitumia, ni njia bora hususani kwa sisi wakulima wa mazao, wakati mwingine husaidia kufanya mazao yaweze kuhifadhika vyema.

Mvua zinapozid tunalazimika kutumia moto kukausha ama kufukizia maoshi ili mavuno yasiharibike, aliongezea Gerard.

Hii ilikuwa moja ya njia maarufu zaidi katika jamii nyingi za Afrika, mazao kama vile Mahindi, mpunga, mihogo, samaki, dagaa, nyama, matunda na mboga zilitandazwa juani hadi kupoteza unyevu. | Picha Natural resource institute

Kutumia Chumvi

Kwa karne nyingi, chumvi imekua ikitumika kufanya shughuli za uhifadhi katika jamii nyingi za kiafrika, ripoti ya utafiti wa SUA inaeleza kuwa mbinu hii husaidia kupunguza unyevu kwenye chakula na kuzuia ukuaji wa baadhi ya vijidudu vinavyosababisha chakula kuharibika.

Mtafiti wa biolojia na dawa kutoka Chuo Kikuu cha Carlifornia, Berkey, Dk Ingrid Koo, anasema chumvi hupunguza molekuli za maji katika chakula na viumbe vyote vilivyo hai vinahitaji maji. Kwa sababu hiyo haviwezi kukua bila maji, ikijumuisha bakteria wanaoweza kusababisha sumu kwenye chakula na kuharibika.

Kwa karne nyingi, chumvi imekua ikitumika kufanya shughuli za uhifadhi katika jamii nyingi za kiafrika, mbinu hii husaidia kupunguza unyevu kwenye chakula na kuzuia ukuaji wa baadhi ya vijidudu vinavyosababisha chakula kuharibika. | Picha MaxiSalt

Kuvundika/usindikaji

Uvundikaji bado ni mbinu muhimu ya jadi nchini Tanzania kwa kuhifadhi mazao, kuongeza thamani na kupunguza upotevu baada ya mavuno. 

Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) inaeleza kuwa mbinu hii hutumika pia kutengeneza vinywaji vya asili kama togwa na mbege ya Wachaga.

Mbinu hii huongeza muda wa kuhifadhi chakula, kuboresha ladha na kuongeza virutubisho kama protini, wanga na bakteria rafiki wanaosaidia mmeng’enyo wa chakula.

Mbinu hii huongeza muda wa kuhifadhi chakula, kuboresha ladha na kuongeza virutubisho kama protini, wanga na bakteria rafiki wanaosaidia mmeng’enyo wa chakula. | Picha Cultures for Health

Kuhifadhi kupitia  vyungu vya udongo 

Vyungu vya udongo vilitumika kuhifadhi maji, maziwa na chakula kutokana na uwezo wake wa kuweka ubaridi wa asili. 

Tovuti ya Hesperian health guides inaeleza kuwa baadhi ya jamii za Afrika pia walitumia mbinu ya vyungu viwili, chungu kidogo huwekwa ndani ya kikubwa, nafasi kati yake ikijazwa mchanga wenye unyevunyevu.

Maji huongezwa mara kwa mara ili mchanga ubaki na unyevu, na chakula huwekwa kwenye chungu cha ndani kikiwa kimefunikwa. Uvukizaji wa maji hupunguza joto na kuifanya mbinu hii kuhifadhi matunda, mboga na vyakula vingine bila umeme.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
10 Aug, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
10 Aug, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
10 Aug, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
EXCLUSIVE: Fahamu ukweli kuhusu kunyonyesha na kumbemenda mtoto | PART 1

EXCLUSIVE: Fahamu ukweli kuhusu kunyonyesha na kumbemenda mtoto | PART 1

Nukta TV

Rais Samia aipa miezi 5 Tume ya Uchunguzi jinai Oktoba 29

Rais Samia aipa miezi 5 Tume ya Uchunguzi jinai Oktoba 29

Nukta TV

Rais Samia ataja sababu kushirikisha wajumbe kutoka nje, Tume ya Uchunguzi makosa ya jinai Oktoba 29

Rais Samia ataja sababu kushirikisha wajumbe kutoka nje, Tume ya Uchunguzi makosa ya jinai Oktoba 29

Nukta TV