Si kweli : Serikali imeongeza likizo ya wanafunzi kwa siku 7

July 1, 2026 5:19 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Serikali yakanusha, yasema shule zitafunguliwa Julai 6, 2026 kama ilivyokua awali.
  • Nukta Fakti yabaini dosari katika barua ikiwemo muundo wa kiutawala, jina na sahihi ya kiongozi mwenye thamana pamoja na ukakasi kwenye sababu za kuongezwa kwa likizo.

Dar es Salaam. Leo katika mitandao ya kijamii kumeibuka mjadala mpana baada ya kusambaa kwa taarifa inayodai kuwa Serikali imeongeza likizo kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kwa siku saba, jambo ambalo sio la kweli. 

Taarifa hiyo iliyotolewa leo Julai 1, 2026 kupitia chapisho feki la barua yenye mfanano na barua kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) ikieleza kuwa shule zitafunguliwa Julai 13, 2026 badala ya Julai 6 mwaka huu kama ilivyopangwa awali. 

Taarifa hiyo imeeleza kuwa sababu za kuongeza kwa likizo hiyo ni kuwawezesha  wanafunzi na walimu kupata mada wa kutosha wa mapumziko. 

“Ofisi ya Rais TAMISEMI inapenda kuwajulisha kuwa, kutokana na uchovu wa likizo kwa wanafunzi, walimu na watumishi wote wa elimu baada ya kipindi kirefu cha mapumziko, imeamua kuongeza siku 7 baadae ya shule kufunguliwa,” inasomeka sehemu ya barua hiyo.

Hata hivyo, timu ya wathibitishaji wa taarifa ya Nukta Fakti imebaini taarifa hiyo sio halali na haijatolewa na mamlaka husika, hivyo wananchi waipuuze.

Mambo yaliyobainika katika taarifa hiyo

Nukta Fakti imebaini dosari kadhaa katika barua hiyo ikiwemo muundo wa kiutawala na ukakasi katika sababu zilizoorodheshwa pamoja na jina na sahihi ya kiongozi mwenye dhamana aliyetoa taarifa husika.

Barua inayosambaa inaonyesha imetoka ‘Ofisi ya Rais Tamisemi’ hata hivyo kwa sasa Tamisemi haiko chini ya Ofisi ya Rais bali Ofisi ya Waziri Mkuu.

Barua pia inaonekana kusainiwa na Waziri wa Elimu, lakini jina na sahihi vilivyopo ni vya Kamishna wa Elimu, Dk Lyabwene M. Mlahabwa, ambaye si Waziri wa Elimu na hana dhamana hiyo. 

Kwa sasa, Waziri wa Elimu ni Adolf Mkenda na Naibu Waziri ni Wanu Hafidh Amer na Katibu Mkuu ni Profesa Carolyne Nombo.

Vilevile barua inadai kuwa uamuzi wa kuongeza likizo umetokana na “uchovu wa likizo” kwa wanafunzi, walimu na watumishi wa sekta ya elimu baada ya kipindi kirefu cha mapumziko, hoja ambayo haina mashiko wala uhalisia wa kiutawala.

Wizara ya Elimu kupitia kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii imekanusha taarifa hiyo, ikibainisha kuwa si ya kweli na kwamba waraka huo haujatolewa na Tamisemi. Katika ufafanuzi wake, wizara imesisitiza kuwa “Taarifa hii si sahihi, ipuuzwe.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
2 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
2 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Msikie Jaji Mkuu Masaju : Mambo wasiopaswa kufanya madalali wa Mahakama.

Msikie Jaji Mkuu Masaju : Mambo wasiopaswa kufanya madalali wa Mahakama.

Nukta TV

Dk Mwigulu: Kama siyo Rais Magufuli mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere usingefanyika

Dk Mwigulu: Kama siyo Rais Magufuli mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere usingefanyika

Nukta TV

Umuhimu wa elimu ya mikopo

Umuhimu wa elimu ya mikopo

Nukta TV