Pauni na Euro zaendelea kuimarika dhidi ya Shilingi ya Tanzania
- Dola ya Marekani na sarafu zingine za kigeni zaendelea kuwa tulivu.
Pauni ya Uingereza pamoja na sarafu ya Umoja wa Ulaya (Euro) zimeonesha kupanda ukilinganisha na siku zilizopita kufuatia ongezeko la thamani ya sarafu hizo katika viwango vya ubadilishaji fedha vilivyotelewa leo Juni 26, 2026 na benki za CRDB na NMB
Kwa mujibu wa benki ya CRDB Euro imenunuliwa kwa Sh2,834.72 kutoka Sh2,826.66 jana na kuuzwa kwa Sh3,134.72 kutoka 3,126.66 ikiwa ni sawa na ongezeko la Sh8.06 sawa na takribani asilimia 0.29, ukilinganisha na siku ya jana.
Kwa upande wa benki ya NMB leo imenunua Euro kwa Sh2,843 na kuuza kwa Sh3,115, ukilinganisha na siku ya jana ambapo Euro ilinunuliwa kwa Sh2,839 na kuuza kwa Sh3,111 sawa na ongezeko la Sh4 sawa na takribani asilimia 0.14.
Kwa ujumla, NMB imeongeza bei ya Euro kwa Sh4 katika viwango vyote vya kununua na kuuza, ongezeko ambalo ni chini ya asilimia 0.2%, ikionyesha mabadiliko kidogo ya soko.Â
Dola ya Marekani imeendelea kuwa tulivu kwa kusalia katika viwango vile vile vya biashara, hali inayoonyesha utulivu wa mahitaji ya sarafu hiyo katika soko la kigeni nchini.
Kwa siku za hivi karibuni sarafu ya Euro imekua ikionesha mabadiliko kutokana na kupanda na kushuka kwa sarafu hiyo dhidi ya shilingi ya Tanzania.
