Serikali yapendekeza kufutwa vocha za kukwangua maeneo ya mijini

June 11, 2026 6:54 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni mkakati wa kuharakisha matumizi ya teknolojia za kidijitali na kuendana na uchumi wa kisasa.

Dar es Salaam. Ili kupunguza matumizi ya fedha taslimu katika mwaka 2026/27 Serikali ya Tanzania imependekeza kusitisha usambazaji na matumizi ya vocha za kukwangua za muda wa maongezi (scratch cards) katika maeneo yote ya mijini yenye miundombinu wezeshi ya malipo ya kidijitali. 

Waziri wa Fedha Khamis Omar aliyekuwa akiwasilisha Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka wa fedha 2026/27 leo Juni 11, 2026 Bungeni jijini Dodoma amesema utekelezaji wa hatua hiyo utafanywa kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). 

“ Serikali pia kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) itaondoa vocha za simu za kukwangua kwa mkono ambapo zoezi hili litaanza katika maeneo yote ya mijini. Hatua hii itasaidia kujifunza kabla ya kutekeleza pendekezo hili kwa maeneo mengine ya nchi,” amesema Balozi Omar. 

Nchini Tanzania, vocha za kukwangua zilianza kuonekana mwishoni mwa miaka ya 1990 na mwanzoni mwa miaka ya 2000 wakati kampuni za simu kama Vodacom Tanzania zilipoanza kutoa huduma za ‘prepaid’ kwa wateja.

Kufikia mwaka 2009, matumizi ya vocha za kukwangua yalikuwa yameenea sana nchini kiasi kwamba watu walikuwa hata wanazitumia kutumiana thamani kama mbadala wa pesa.

Licha ya pendekezo hilo la Serikali, baadhi ya watoa huduma tayari walishaanza kutekeleza utaratibu huo hata kabla ya ya pendekezo hili kutolewa, baada ya kuanza kupoteza watumiaji wa huduma zao.

Hata hivyo, iwapo agizo hilo litapitishwa rasmi, wauzaji na wanunuzi watalazimika kutumia njia mbadala za malipo, ikiwemo vocha za kurusha salio, M-Pesa, Mixx by Yas pamoja na huduma nyingine za kibenki zitakazowawezesha kufanya miamala kwa urahisi zaidi.

Ukiachana na hilo, pendekezo lingine ni kuweka sharti la kufungua akaunti ya benki kama moja ya vigezo vya utoaji wa leseni kwa wafanyabiashara wanaoshiriki katika shughuli za madini, mifugo, mazao, mbao na uvuvi.

Pia, kuhakikisha miamala inafanyika kupitia akaunti husika na kuweka sharti la uthibitisho wa malipo ya kidijitali kuwa rejea ya lazima itakayotumika kuidhinisha maombi ya uhamishaji wa mali kama vile ardhi, majengo na magari.

Vilevile, kuweka sharti la baadhi ya malipo ya huduma na biashara kufanyika kwa njia za kidijitali , pamoja na kuweka sharti la matumizi ya vifaa vya malipo ya kidijitali (Lipa Namba na TANQR) kama moja ya kigezo wakati wa utoaji na uhuishaji wa leseni ya biashara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
14 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
14 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
14 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV