Rais Samia: matumizi ya gesi ni jambo la lazima

February 3, 2024 3:03 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Aagiza matumizi ya gesi majumbani.
  • Asema matumizi ya gesi sio anasa.

Rais Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya nishati ya gesi nchini kwa sasa ni suala la lazima kutokana na faida mbalimbali ikiwemo za utunzaji mazingira na afya.

Kiongozi huyo wa nchi aliyekuwa akizungumza katika hafla ya utiaji saini mikataba ya mauziano na uendeshaji wa kitalu cha Mnazi Bay amewaambia wahudhuriaji kuwa kutokana na kuogezeka kwa elimu juu ya matumizi ni vyema kwa jamii kuhamia katika matumizi ya nishati hiyo.

“Tulikuwa tunatishana kwamba ukiweka gesi utalipuka nyumba pamoja na wanao…tulipofika hapa hili ni jambo la lazima, sasa majumbani kwetu kwingi tutumie gesi,” amesema Rais Samia Ikulu jijini Dodoma leo Februari 3, 2024.

Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Mussa Makame (kulia) pamoja na Meneja Mkazi wa M & P Exploration Production Tanzania Limited Nicolas Engel (kushoto) wakisaini Mkataba wa Mauziano ya Hisa katika Kitalu cha uzalishaji wa Gesi Asilia cha Mnazibay.Picha|Ikulu.

Aidha, kiongozi huyo amesema kuwa ajenda ya matumizi ya nishati hiyo si ya Tanzania pekee bali ni ya bara zima la Afrika na kwamba atatumia nafasi yake kama kionngozi kuhamasisha matumizi ya nishati hiyo.

“Kama mkuu wa nchi nimebaba ajenda hii kwa Afrika kutoa nishati safi na salama kwa wanawake wa Afrika ili wapike kwa nishati safi na salama…

…Suala la kuwa gesi sio anasa kama Serikali tunawajibika kutoa huduma hiyo kwa wananchi kupitia sekta binafsi,” amesema Rais Samia.

Kauli ya Rais Samia ni muendelezo wa harakati za Serikali kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia ambapo lengo ni kufikia asilimia 80 ifikapo mwaka 2030.

Ili kufikia lengo hilo Serikali iliahidi kuweka nguvu kubwa kutoa elimu na uwekeza katika kuwezesha upatikanaji wa nishati safi maeneo ya  vijijini ambapo shughuli kubwa za ukataji miti kwa ajili ya mkaa na kuni hufanyika.

Jitihada hizo zitaiokoa Tanzania dhudi ya  athari za uharibifu wa mazingira na pia kupambana na athari za mabadiliko yanaendelea nchini na duniani kote.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV