Jinsi ya kupika spinachi

December 17, 2024 3:18 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Pishi hili ni chanzo kizuri cha virutubisho katika mwili wa binadamu.
  • Hakikisha mboga haipikwi kwa muda mrefu ili isiondoe virutubisho.

Wapenzi wa mboga za majani leo tumewafikia, tutajifunza kwa pamoja jinsi ya kuandaa mboga ya spinach iliyonakshiwa viungo mbalimbali ikiwemo karoti ambayo huongeza ladha na vitamini mwilini.

Inawezekana hupendi mboga za majani ila kwa aina hii ya mapishi hakika utaipenda na unaweza pia kuwaandalia watoto au wageni watakaokutembelea.

Mbali na ladha tamu Spinachi ina wingi wa vitamini A, K, C, B6 na potassium ambavyo Taasisi ya chakula na Lishe Tanzania (TFNC) inabainisha kuimarisha kinga mwili.

Namna ya kuandaa hatua kwa hatua

Hatua ya kwanza katika chombo kisafi chenye maji osha mboga za spinachi, karoti na kitunguu maji ili kuondoa mchanga na uchafu kwenye mboga.

Baada ya kuosha endelea kwa kukata mboga kwa kuzingatia muongozo wa uaandaaji chakula kama inavyoshauriwa na wataalamu kisha hamia kwenye karoti na vitunguu maji ambavyo utavikata katika vipande virefu vyembamba.

Maandalizi yakikamilika anza kwa kuwasha jiko na itapendeza zaidi ukitumia nishati safi ya kupikia ikiwemo gesi na jiko la umeme ambalo litaharakisha mapaishi na kutunza virutubisho vya mboga za majani.

Endelea na mapishi kwa kubandika sufuria na ikipata moto weka mafuta ya kupikia yakifuatiwa na kitunguu maji utakavyopika kwa dakika mbili hadi viwe na rangi ya kahawia.

 Weka spinachi zilizokatwa katawa na kuoshwa vizuri ikifuatiwa na binzari, garam masala na uzifunike kwa dakika tatu kisha uendelee kwa kuweka  karoti pamoja na chumvi na uzifunike kwa dakika nyingine nne ziive.

Hakikisha mboga zako hazikai kwa muda mrefu jikoni ili zisipoteze ladha na virutubisho vinavyohitajika, unaweza kuongeza nazi na pilipili kama unapendelea.

Mpaka hapo mboga ya spinachi ipo tayari kwa kuliwa na unaweza kuila kwa ugali, wali ama chapati.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Nukta TV

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Nukta TV

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Nukta TV