Jinsi ya kutengeneza Mocktail ya Blue Ocean

December 23, 2024 4:50 pm Ā· Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Unaweza kutengeneza kinywaji hiki kwa ajili ya biashara au matumizi binafsi.
  • Kinywaji hiki hakina mchanganyiko wa kileo hivyo kinafaa kwa matumizi ya rika zote.Ā 

Katika msimu huu wa sikukuu za mwisho wa mwaka watu wengi hujaribu kuandaa vyakula na vinywaji vya tofauti ili kuvutia wageni na wanafamilia ambao hujumuika pamoja kwa ajili ya kusherekea.

Kati ya vinywaji vingi vilivyopo duniani unavyoweza kuandaa katika msimu basi Mocktail ya Blue Ocean ndiyo yenyewe.

Kinywaji hiki ambacho hakitengenezwi na aina yoyote ya pombe huvutia wengi kutokana na rangi yake ya kuvutia inayotokana na shira ya Blue CuraƧao yenye ladha ya machungwa pamoja na soda au juisi nyingine za machungwa.

Jiko Point leo imekusogezea njia rahisi ya kutengeneza mocktail ya Blue Ocean ukiwa nyumbani ambapo unaweza kuokoa Sh 12,000 mpaka 20,000 kwa kila glasi kama ungenunua kinywaji hicho katika maeneo ya starehe

Kama ulikuwa hujui Mocktail ni mchanganyiko wa vinywaji na viungo

Hatua ya kwanza ni kuandaa mahitaji ikiwemo  glasi au chombo chochote kikubwa utakalolitumia kuwekea kinywaji chako mara baada ya kuiandaa, kisha andaa vipande vya barafu (kulingana na mahitaji), shira ya Blue Curaçao juisi ya machungwa na soda ya limao.

Shira ya Blue CuraƧao inapatikana katika maduka yote yanaouza vinywaji na huuzwa kuanzia Sh18,000 mpaka Sh36,000 kulingana na ujazo.

Katika maandalizi anza kwa kuweka vipande vya barafu kiasi katika glasi au chombo kikubwa utakachokitumia ikifuatiwa na shira ya Blue CuraƧao mililita 30 na juisi ya machungwa mililita 30 kisha malizia na soda ya limao au soda ya sprite mililita 90.

Baada ya hapo koroga taratibu mchangavyiko wako mpaka kinywaji chako kichanganyike vizuri na kupata rangi nzuri ya blue bahari kisha kitakuwa tayari kwa kunywa,

Pamba glasi yako kwa kipande cha chungwa kufanya kinywaji chako kuwa na muonekano wa kuvutia.Ā 

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jun, 2026 Ā· TZS
No gainers today
No losers today
5 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Unaweza kusema ni maumivu juu ya maumivu kwa watumiaji wa vyombo vya moto vinavyotumia mafuta ya

Unaweza kusema ni maumivu juu ya maumivu kwa watumiaji wa vyombo vya moto vinavyotumia mafuta ya

Nukta TV

Neema Mohamed, Mkurugenzi wa Bone and Blood Foundation, ni shujaa wa ugonjwa wa selimundu Sickl

Neema Mohamed, Mkurugenzi wa Bone and Blood Foundation, ni shujaa wa ugonjwa wa selimundu Sickl

Nukta TV

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ametua kwenye ardhi ya Urusi kwa ziara ya kitaifa ya siku

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ametua kwenye ardhi ya Urusi kwa ziara ya kitaifa ya siku

Nukta TV