Jinsi ya Kutengeneza Cocktail ya Blue Lagoon

December 20, 2024 5:52 pm Ā· Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Rangi ya samawati pamoja na ladha ya machungwa hufanya kinywaji hicho kivutie zaidi.
  • Kinywaji hiki hutengenezwa kwa pombe hivyo hakifai kutumiwa na watoto, wajawazito na wagonjwa.

Blue Lagoon niĀ  mojawapo ya cocktail zinazopendwa zaidi duniani, ikiwa na sifa adimu ikiwemo rangi samawati angavu inayofanana na bahari safi pamoja na mchanganyiko wa barafu ambao huburudusha wanywaji wake.

Huenda umaarufu wake umetokana na mchanganyiko unaounda kinywaji hicho ambao ni limao, ladha ya machungwa kutoka kwenye kinywaji kingine kinachoitwa ā€˜Blue CuraƧao’ ikisindikizwa na aina mbalimbali ya pombe ikiwemo Vodka.

Kama ulikuwa hufahamu Cocktail ni mchanganyiko wa vinywaji vya pombe na vinywajiĀ  vingine kama juisi, sharubati, au matunda hivyo uwepo wake ndiyo unaotoa ladha na maana ya kinywaji tunachokiandaa leo.

Ikiwa wewe ni mtembeleaji wa sehemu za starehe bila shaka umewahi kukutana na kinywaji hiki ambacho bei yake huanzia Sh 18,000 hadi Sh35,000 kwa glasi kutegemeana na sehemu ulipokinunua.

Ili kufurahia utamu wa kinywaji hicho, jiko point imekusogezea maandalizi rahisi ya kukiandaa nyumbani ili uweze kukifurahia pamoja na uwapendao.

Kumbuka kinywaji hiki kinatengenezwa kwa pombe hivyo hakifai kutumiwa na watoto, wajawazito na wagonjwa.

Namna ya kuandaa hatua kwa hatua

Weka kiasi kidogo cha vipande vya barafu (Ice Cubes) katika glasi ikifuatiwa na viipande vya limao (lemon slice) kisha uongeze aina yoyote ya Vodka uipendayo auĀ  watakayochagaua wageni wako.

Katika glasi hiyo hiyo mimina Blue CuraƧao kiasi mililita 30 ikifuatiwa na soda ya limao na kijiko kimoja cha maji ya limoa ili kuongeza aladha.

Ā haujazi hakikisha unamimina vinywaji hivyo taratibu ili kutengeneza matabaka ya rangi yakayoborhs amuonekano wa kinywaji chako.

Pamba kwa kipande cha limao pamoja na cheri juu ya glasi na baada ya hapo kinywaji chako kitakuwa tayari kwa ajili ya matumizi.

Usikose kuendelea kufuatilia makala zetu kwa maandalizi ya vinywaji vya kuvutia.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
25 Jun, 2026 Ā· TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
25 Jun, 2026 Ā· TZS
No gainers today
No losers today
25 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Zungu: Kura zimepigwa , pesa ya Serikali imeruhusiwa kuanza sasa kuitumia

Zungu: Kura zimepigwa , pesa ya Serikali imeruhusiwa kuanza sasa kuitumia

Nukta TV

Bunge la Tanzania lapitisha ya Serikali kwa 97%

Bunge la Tanzania lapitisha ya Serikali kwa 97%

Nukta TV

Hawa hapa wabunge waliopiga kura ya hapana, kupitisha Bajeti ya Serikali

Hawa hapa wabunge waliopiga kura ya hapana, kupitisha Bajeti ya Serikali

Nukta TV