Juisi ya karoti na ndizi

August 26, 2025 5:38 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Kwa wale wanaosumbuliwa na matatizo ya choo kigumu, au watoto wanaoanza kula juisi hii inawafaa.
  • Utahitaji ndizi na karoti tu ili kuandaa kinywaji hiki.

Huenda umeshawahi kunywa aina nyingi za juisi zenye ladha tofauti na zilizoburudisha koo lako na kukufanya kila mara utamani kujua jinsi zinavyotengenezwa.

Sasa katika orodha yako ya aina ya juisi ulizowahi kunywa ongeza na juisi ya karoti na ndizi itakayokuburudisha huku ikikupa faida lukuki za kiafya.

Juisi ya karoti na ndizi ni kinywaji chenye afya, kitamu na rahisi kuandaa kinachokupa nguvu na virutubisho muhimu katika mwili ikiwepo nyuzi nyuzi na vitamini A zinazosaidia kudhibiti mmeng’enyo wa chakula na afya ya ngozi.

Na kwa kuona umuhimu wa juisi hii leo JikoPoint.co.tz inakusogezea hatua kwa hatua namna ya kuandaa ukiwa nyumbani.

Mahitaji

  • Ndizi 3
  • Karoti kubwa 3
  • Maji ¼ robo lita
  • Mdalasini (hiari sio lazima)

Hatua kwa hatua namna ya kuandaa

Hatua ya kwanza osha karoti na ndizi kwa maji safi kisha uanze kumenya na kukatakata kwa saizi ndogo itakayoweza kusagika kwa haraka.

Baada ya hapo andaa blenda na uweke karoti kwanza kisha uzisage na maji  upate juisi nzito.

Kama unatumia juicer basi unachopaswa kufanya ni kusaga karoti ambazo baada ya hapo utachuja kwa chujio ili kupata juisi nzuri ambayo hutohitaji kusaga.

Hatua nyingine ni kuchukua ndizi na juisi ya karoti kisha kusaga kwa pamoja mchanganyiko huo ambao utatumia dakika 2 mpaka dakika 4 utakuwa umepata juisi tamu na nzito.

Ikiwa unapenda viungo unaweza kuongeza mdalasini wa unga unafaa ingawa sio lazima.

Kama juisi ni nzito ongeza maji au maziwa kidogo hadi upate uzito unaoupenda.

Mpaka hapo juisi yako sasa iko tayari. Unaweza kuihifadhi kwenye jokofu na kunywa bila kuongeza sukari kwani karoti na ndizi tayari zina sukari asilia.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
12 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
12 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

Nukta TV

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Nukta TV

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Nukta TV