Hatua kwa hatua utengenezaji wa juisi ya parachichi na nazi

December 4, 2024 12:28 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Juisi hii ina wingi wa vitamini ikiwemo E, K na C.
  • Husaidia kudhibiti shinikizo la damu na kufanya mapigo ya moyo kuwa ya kawaida.

Je unajua utamu wa juisi ya parachichi na nazi? 

Kama bado ni muhimu kuelewa kuwa juisi ya parachichi na nazi ni kinywaji cha asili chenye ladha tamu na manufaa kwa afya yako. 

Kwa mujibu wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) juisi ya matunda halisi huupatia mwili vitamini na makapimlo yaliyo kwenye matunda halisi husaidia kupunguza uwezekano wa kuugua saratani ya utumbo.

Matunda haya licha ya kutumika katika mazingira ya kila siku yana wingi wa vitamini E, K, B na C, na madini ya potasiamu.  Husaidia kudumisha afya na kudhibiti shinikizo la damu na kufanya mapigo ya moyo kuwa ya kawaida.

Na leo ndani ya jikopoint.co.tz tunaenda kujifunza namna ya kuandaa juisi hii ambayo ni fursa kwa wafanyabiashara na matumizi ya nyumbani. 

Hatua kwa hatua 

Hatua ya kwanza katika utengenezaji wa juisi hii ni kuosha matunda kwa kutumia maji safi na salama ili kuondoa uchafu. Menya parachichi na uondoe mbegu kisha kata vipande vidogo ili iwe rahisi kusaga.

Hatua inayofuata tengeneza tui la nazi kulingana na kiasi cha juisi. Hakikisha unapata tui zito. 

Andaa blenda ya kusaga kisha weka vipande vya parachichi na ongeza tui la nazi, asali na maji ya ndimu au limao. Ukipenda unaweza kuongeza unga wa mdalasini.

Ukimaliza hatua hiyo saga mchanganyiko wote kwa sekunde 30 hadi 60 mpaka uwe laini na ikiwa unataka juisi iwe nyepesi ongeza maji kiasi kisha saga kwa dakika 3 hadi 5.

Mpaka hapo juisi ya parachichi na nazi inakuwa tayari kwa kunywa. Unaweza kuongeza vipande vya barafu au kuweka kwenye jokofu kwa ajili ya matumizi ya baadaye. 

Usisubiri kusimuliwa tengeneza leo ufurahie ladha tamu!

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
25 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
25 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Zungu: Kura zimepigwa , pesa ya Serikali imeruhusiwa kuanza sasa kuitumia

Zungu: Kura zimepigwa , pesa ya Serikali imeruhusiwa kuanza sasa kuitumia

Nukta TV

Bunge la Tanzania lapitisha ya Serikali kwa 97%

Bunge la Tanzania lapitisha ya Serikali kwa 97%

Nukta TV

Hawa hapa wabunge waliopiga kura ya hapana, kupitisha Bajeti ya Serikali

Hawa hapa wabunge waliopiga kura ya hapana, kupitisha Bajeti ya Serikali

Nukta TV