Vodacom inavyoimarisha ulinzi wa taarifa binafsi kukabili utapeli mtandaoni

February 18, 2026 7:44 am · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Yaendelea kudumisha mifumo ya uendeshaji huduma ikitoa elimu kwa wateja kuhusu namna ya kuepuka utapeli wa mitandaoni.

Dar es Salaam. Kampuni ya mawasiliano ya simu ya Vodacom Tanzania imesema inaendelea kuimarisha ulinzi wa taarifa binafsi kwa wateja wake ili kudhibiti vitendo vya utapeli wa mitandao.

Mkuu wa masuala ya sheria na ulinzi wa taarifa binafsi wa Vodacom, Jacqueline Kalaze aliyekuwa akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam Februari 17, 2026, amesema amesema kulinda taarifa binafsi za wateja ni jambo la msingi linalohakikisha faragha ya mteja inaheshimiwa na kuzuia taarifa hizo kutumiwa vibaya hususan kwenye vitendo vya utapeli wa mitandao.

“Matapeli wa mtandaoni hawawezi kufanya utapeli endapo hawana taarifa zako binafsi, ndiyo Vodacom tunaweka mkazo mkubwa katika kulinda na kudhibiti usalama wa taarifa za wateja wetu ili zisitumike vibaya,” amesema Kalaze.

Taarifa binafsi ni taarifa yoyote inayomtambulisha mtu moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja, ikijumuisha jina, namba ya kitambulisho, alama za vidole, picha, taarifa za kifedha, afya, au vinasaba (DNA). 

Vodacom kuwa miongoni mwa kampuni tatu za kwanza kusajiliwa na Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) tangu kuanza kutekeleza sera hiyo mwaka 2018 ikiwa kama kampuni inayofanya kazi katika nchi nyingi (multi-country company). Picha | Bongo5

Kwa mujibu wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi Na. 11 ya 2022, taarifa hizi zina umuhimu mkubwa kwa mhusika, hivyo ni lazima zilindwe na kutumika kwa pale tu muhusika anapoidhinisha. 

Miongoni mwa juhudi zinazotumiwa na Vodacom ni pamoja na kuhakikisha inakuwa na mifumo imara kwa kutoa nafasi kwa wataalamu ikiwemo wanafunzi wa vyuo vikuu kuweza kubaini mianya iliyopo ili kuthibitisha usalama wake na kuondoa hatari zozote zinazoweza kuweka taarifa za wateja katika hatari ya kudukuliwa.

Kwa mujibu wa Isambo Binde, Mkuu wa Idara inayohusiana na masuala ya Hatari na Usalama wa kampuni hiyo, amefafanua kuwa hata mifumo ya uendeshaji ya Vodacom hairuhusu wafanyakazi kuona taarifa nyeti za mteja kama vile namba ya siri ili kuhakikisha taarifa hizo zinalindwa.

“Taarifa zote zipo ‘encrypted’ na ndio maana mtoa huduma huuliza taarifa zako kama namba ya Nida kwa sababu hawezi kuziona na hawezi kufanya chochote bila idhini ya mtumiaji” amesema Isambo Binde, Mkuu wa Idara inayohusiana na masula ya hatari na usalama wa Vodacom.

Elimu dhidi ya utapeli mtandaoni hutolewa

Mbali na kuboresha mifumo Vodacom imekuwa ikifanya juhudi za kutoa elimu kwa wateja kwa kutuma ujumbe mfupi (SMS), kuandaa warsha, na mafunzo mbalimbali yanayolenga kuwajengea uelewa juu ya usalama wa kidijitali.

Mbinde amebainisha kuwa ndani ya mwezi mmoja Vodacom hutuma zaidi ya SMS milioni 20 zinazowatahadharisha na kutoa elimu kwa wateja juu ya utapeli wa mtandao.

Juhudi hizo zimeifanya Vodacom kuwa miongoni mwa kampuni tatu za kwanza kusajiliwa na Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) tangu kuanza kutekeleza sera hiyo mwaka 2018 ikiwa kama kampuni inayofanya kazi katika nchi nyingi (multi-country company).

Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) wa kampuni ya huduma za mawasiliano ya Vodacom Plc, Athuman Mlinga (kulia) akipokea tuzo kutoka kwa Katibu wa Chama cha kitaaluma cha kimataifa cha Ukaguzi na Udhibiti wa Mifumo ya Habari (Isaca), Rosevita Majani, Juni 2025. Picha | Mwananchi.

Jitihada za Vodacom huenda zikasaidia kupunguza idadi ya utapeli mtandaoni husasan katika kipindi hiki ambacho matumizi ya mitandao na simu za mkononi yanazidi kuongezeka.

Kwa mujibu wa Ripoti ya Takwimu za Uhalifu na Matukio ya Usalama Barabarani ya mwaka 2024 zilionyesha kuwa matukio ya utapeli yaliongezeka mara mbili zaidi katika kipindi cha mwaka mmoja.

Ripoti hiyo iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na Jeshi la Polisi inabainisha kuwa mwaka 2023 matukio 57 ya utapeli mtandaoni yalirekodiwa idadi iliyoongezeka kufikia matukio 137 mwaka jana. 

Aidha, matukio ya utapeli wa fedha kwa kutumia mitandao ya simu au kutoa fedha kutoka benki na kwenye mashine za kutolea pesa (ATMs) nayo yaliongezeka kwa asilimia takriban 10 ndani ya mwaka mmoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow Us on TikTok

Subscribe to Our YouTube Channel

Subscribe

Loading videos...

Loading videos...

Loading videos...

Enable Notifications OK No thanks