Barabara ya njia nne Tengeru – Arusha kumuenzi Edwin Mtei

January 24, 2026 4:33 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Mbali na ujenzi wa barabara, Mtei pia ataenziwa kwa kusimamia haki na maendeleo ya wananchi na kutatuliwa kwa haki mgogoro wa ardhi.

Dar es Salaam. Serikali imeagiza kuharakishwa kwa ujenzi wa barabara ya njia nne kutoka Tengeru hadi Arusha kama sehemu ya kumuenzi mzee Edwin Mtei kwa vitendo

Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba aliyekuwa akitoa Salam za pole leo Januari 24,2025 katika mazishi ya Mtei, amesema maelekezo hayo yametolewa na Rais Samia Suluhu kuhakikisha mchango wa mzee Mtei unaenziwa kwa vitendo vinavyoonekana. 

“Nitumie jukwaa hili kumuagiza Waziri wa Fedha na Waziri wa Ujenzi kuhakikisha ujenzi wa barabara ya njia nne kutoka Tengeru hadi KIA unakamilika mara moja…

…Kazi ianze haraka kama ishara ya kumuenzi Mtei, ambaye ametukusanya hapa leo,” amesema Waziri Mkuu huku akisisitiza ifikapo Februari 20, 2026 barabara hiyo iwe imefunguliwa. 

Hii sio mara ya kwanza kwa Serikali kuahidi kukamilisha ujenzi wa barabara ya njia nne katika jiji la Arusha licha ya umuhimu wake katika kukuza shughuli za utalii zinazoendelea jijini humo.

Ujenzi wa barabara hiyo kuanzia uliogawanywa kwa vipande vipande kutoka Arusha hadi Holili mkoani Kilimanjaro kwa mara ya kwanza iliahidiwa na Rais John Pombe Magufuli mwaka 2016.

Tangu wakati huo barabara imekuwa ikikamilishwa kwa awamu ila kipande cha Tengeru ambapo ndipo palipokuwa nyumbani kwa mzee Mtei hadii eneo la USA jijini humo palipoahidiwa njia nne bado hapajakamilika.

Julai 26, 2022, aliyekuwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, alisema awamu ya pili ya ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami, kwa kipande cha Tengeru–USA River yenye urefu wa kilometa 11.3 unaendelea.

Hata kufikia Januari 5, 2025 Meneja wa Uboreshaji wa Barabara ya Arusha-Holili, Manger Rajab aliyekuwa akizungumza mbele ya Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega alisema wameshaanza mchakato wa kuwapata wakandarasi ambao wataanza kuingia eneo la mradi Machi, 2025.

Kukamilika kwa ujenzi wa barabara hizo jijini Arusha kunatarajiwa kupunguza foleni isyokuwa na ulazima ikitoa nafasi ya kufanyika kwa shughuli za utaliii zitakazokuza uchumi wa nchi.

Mbali na ujenzi wa barabara, Waziri Mkuu amesema kumuenzi Edwin Mtei kunapaswa kujumuisha kusimamia haki na maendeleo ya wananchi, kutatuliwa kwa haki mgogoro wa ardhi wa Shamba la Mringa Estate na kuboreshwa kwa mazingira ya wafanyabiashara wadogo, wakiwemo wamachinga, katika Jiji la Arusha.Nae Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) John Heche amesema chama hicho kitaendelea kumkumbuka Mtei kama mfano wa kiongozi aliyesimamia misingi ya haki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow Us on TikTok

Subscribe to Our YouTube Channel

Subscribe

Loading videos...

Loading videos...

Loading videos...

Enable Notifications OK No thanks