Tanzania kinara idadi ya Simba Afrika

Shirika la World Population Review limeitaja Tanzania kuwa na simba 14,500 idadi inayoifanya kuwa kinara wa idadi kubwa ya Simba barani Afrika.
Katika mbuga zake za kitaifa na mapori ya akiba nchini Tanzania, unaweza kuona simba jike wakiwinda alfajiri, madume wakinguruma na wengine wakiwinda au kupumzika katika vivuli vya miti.
Unaweza kujionea wanyama hao katika hifadhi mbalimbali ikiwemo Serengeti, Ngorongoro, Tarangire na Ruaha.
Hata hivyo, takwimu hizo zinatofautiana na zile zilizotolewa na IUCN pamoja na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) ambao waliripoti idadi ya simba hao kuwa 17,000.
Nchi nyingine yenye idadi kubwa ya simba ni Afrika Kusini (Simba 3,284), Botswana (Simba 3,063), Kenya (Simba 2,515) na Zambia (Simba 2,500)
Pamoja na hayo, Tawiri ilibainisha kuwa Tanzania imeongoza barani Afrika kwa kuwa na idadi kubwa ya wanyama wengine ikiwemo Nyati na Chui.
Latest