Malaria bado ni tishio duniani, maambukizi yaongezeka

December 5, 2025 4:00 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Kesi mpya zafikia milioni 282
  • WHO yaeleza sababu.

Dar es Salaam. Licha ya hatua kubwa zilizopigwa katika kukabiliana na malaria duniani, ugonjwa huo umeendelea kuwa tishio huku visa na vifo vikiongezeka katika maeneo mengi, hususan barani Afrika.

Ripoti ya Malaria iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO), Desemba 4,2025, inabainisha kuwa mwaka 2024 kulikuwa na takribani kesi milioni 282 za malaria duniani kote.

Idadi hiyo ni sawa na ongezeko la kesi milioni 9 ( asilimia 3.3) kutoka kesi milioni 273 ziliripotiwa mwaka 2023.

Kwa upande wa Tanzania WHO imesema mwaka 2024 kulikuwa na kesi milioni 9.4 za Maralia zilizoripotiwa.

Takwimu hizo zinatofautiana na za Wizara ya Afya Tanzania zilizolotolewa  Aprili 25,2025 zikionyesha visa milioni 3.3 ya malaria ikiwa ni ongezeko la asilimia 184 kulingaisha na visa vilivyoripotiwa mwaka 2023.

Mbali na Tanzania, WHO imeripoti visa vipya vya malaria katika nchi nyingine za Afrika ikiwemo Nigeria, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Uganda,Ethiopia na Msumbiji.

Vifo vyaongezeka, WHO yaeleza sababu

Mwaka 2024, WHO inaeleza kuwa watu 610,000 walipoteza maisha kutokana na ugonjwa wa malaria, sawa na ongezeko la vifo 12,000 ukilinganisha na vifo 598,000 vilivyolipotiwa mwaka 2023.

Hii ni sawa na ongezeko la asilimia 2.01 ya vifo vilivyotokea mwaka 2023.

Kwa mujibu wa malengo ya kimataifa, kiwango kinachotakiwa ni vifo 4.5 kwa watu 100,000, lakini mwaka 2024 idadi ya vifo ilizidi kiwango hicho na kufikia 13.8 ikiwa ni mara tatu zaidi ya lengo.

Kwa mwenendo huu, WHO inaonya kuwa kufikia 2030, vifo vinaweza kuwa mara tisa ya lengo ikitaja ufinyu wa ufadhili kimataifa kama sababu.

Mwaka 2024, Dola za Marekani bilioni 9.3 (Sh22.6 trilioni) zilihitajika kudhibiti ugonjwa wa malaria, lakini kiasi kilichowekezwa ni Dola za Marekani bilioni 3.9 sawa na (Sh9.5 trilioni).

Kiasi hiicho ni pungufu ya asilimia 41 ya lengo lililowekwa ili kupambana na ugonjwa huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow Us on TikTok

Subscribe to Our YouTube Channel

Subscribe

Loading videos...

Loading videos...

Loading videos...

Enable Notifications OK No thanks