Wizara ya Elimu yatangaza ufadhili wa masomo Russia

October 9, 2025 5:42 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Ufadhili huo utahusisha ada pekee.
  • Dirisha la kutuma maombi hayo litafungwa rasmi Januari 16, 2026

Arusha. Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeutangazia umma kuhusu fursa mpya ya ufadhili wa masomo ya elimu juu nchini Russia katika mwaka wa masomo 2026/27.

Taarifa ya Wizara ya Elimu iliyotolewa leo Oktoba 9, 2025 inabainisha kuwa ufadhili huo utahusisha ada ya masomo pekee na muombaji atatakiwa kugharamia mahitaji mengine muhimu.

“Huu ni udhamini wa sehemu. Utagharamia ada ya masomo pekee na waombaji watawajibika kukidhi gharama za malazi, gharama za usafiri, huduma ya afya/bima, vifaa vya kuandikia na ada za visa…

…Serikali ya Tanzania haitoi msaada wowote wa mkopo au ruzuku kwa watakaopata ufadhili huu,” imesema taarifa hiyo.

Dirisha la kutuma maombi hayo litafungwa rasmi Januari 16, 2026 ikitoa nafasi kwa wanafunzi wa kitanzania wenye ndoto za kusoma nje ya nchi kutuma maombi ya ufadhili huo.

Ili kupata fursa hiyo mwombaji atatakiwa kuwa na cheti ya kumalizia elimu ya Sekondari (CSEE) na cheti cha kidato cha sita (ACSEE) chenye ufaulu wa  kiwango cha chini cha divisheni II au cheti cha Diploma chenye ufaulu wa GPA isiyopungua 3.5 katika fani zinazohusiana.

“Mwombaji awe na Shahada ya kwanza ya sanaa/ shahada ya sayansi na GPA isiyopungua 3.5 (kwa waombaji wa shahada ya uzamili)…awe na Shahada ya Uzamili (kwa waombaji wa shahada ya uzamivu PhD,”imefafanua taarifa ya Wizara ya Elimu ikizitaja sifa nyinginezo za mwombaji.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ili kukamilisha maombi hayo, mwombaji atatakiwa kuwasilisha nakala za vyeti vya kitaaluma na nakala zilizochanganuliwa (scanned) za ukurasa wa biodata ya pasipoti.

Mchakato wa maombi na uwasilishaji

Waombaji wanapaswa kujiandikisha na kujaza fomu ya maombi ya mtandaoni kwa kupitia tovuti ya https://education-in-russia.com huku maelekezo muhimu ya maombi ya ufadhili huo na program za masomo yakipatikana kupitia tovuti ya https://studyinrussia.ru/en/

Baada ya kujaza sehemu zote zinazohitajika, mwombaji atatakiwa kutuma maombi yake mtandaoni kwa kubofya kitufe cha kijani ikiashiria kukamilika kwa mchakato wa maombi hayo na yale yatakayotumwa nje ya mfumo.huo hayatapokelewa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow Us on TikTok

Subscribe to Our YouTube Channel

Subscribe

Loading videos...

Loading videos...

Loading videos...

Enable Notifications OK No thanks