Hitilafu mfumo wa malipo yasababisha changamoto manunuzi ya umeme nchini

October 2, 2025 3:24 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Hitilafu hiyo imesababisha huduma zote za ununuzi wa umeme kupitia mitandao ya simu, mawakala na benki kutokuwa na ufanisi.

Dar es Salaam. Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limesema changamoto ya manunuzi ya umeme (LUKU) iliyotokea siku za hivi karibuni imesababishwa na  hitilafu kwenye Mfumo wa Malipo ya Serikali (GePG).

Hali hiyo imesababisha malalamiko miongoni watumiaji wa huduma ya umeme kwa kuwa ndio nishati inayotegemewa kwa kiasi kikubwa kufanikisha shughuli za kiuchumi kama uchakataji wa bidhaa katika viwanda vidogo.

Aidha, wajasiriamali wanaotegemea umeme kuhifadhi bidhaa zao kama mama lishe na wanaouza bidhaa oza (matunda, nyama) watatakiwa kutafuta nishati mbadala ili kuepuka hasara ya kuharibikiwa na bidhaa zao mpaka pale huduma zitakaporejea.

Kwa mujibu wa taarifa ya iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano na Huduma kwa Wateja Tanesco, hitilafu hiyo imesababisha huduma zote za ununuzi wa umeme kupitia mitandao ya simu, mawakala na benki kutokuwa na ufanisi.

“Changamoto hii inasababishwa na hitilafu kwenye mfumo wa malipo ya Serikali (GePG). Tayari  wataalamu wa GePG wanashughulikia changamoto iliyojitokeza ili huduma iweze kurejea katika hali ya kawaida,” imeeleza taarifa hiyo.

Aidha,Tanesco imetoa wito kwa wataalamu wa GePG kushughulikia tatizo hilo kwa haraka ili kuwaondolea wateja usumbufu ikiongeza kuwa itawafahamisha wateja wake pale huduma zitakaporejea kikamilifu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow Us on TikTok

Subscribe to Our YouTube Channel

Subscribe

Loading videos...

Loading videos...

Loading videos...

Enable Notifications OK No thanks