Utalii waongeza fedha za kigeni Tanzania
- Mapato yafikia Sh9.5 bilioni
Arusha. Hifadhi ya fedha za kigeni ikiwemo Dola za Marekani imeendelea kuongezeka nchini, kutokana na kuongezeka kwa shughuli za utalii katika maeneo mbalimbali nchini.
Ripoti ya ya uchumi ya kila mwezi inayotolewa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Kwa mwaka ulioishia Julai 2025, imebainisha kuwa mapato yatokanayo na shughuli za utalii yamefikia Dola za Marekani milioni 3.8 sawa na Sh9.5 bilioni.
Fedha hizo ni sawa na asilimia 23.2 ya Sh 9 bilioni (Dola za Marekani 16.5 milioni) zilizopatikana baada ya mauzo ya bidhaa na huduma nje ya nchi kwa mwaka ulioshia Julai 2025.
Katika mwaka ulioishia Julai 2024 mapato yatokanayo na shughuli za utalii yalifikia Sh8.7 bilioni (Dola za Marekani 3.5 milioni) ikiwa ni kiwango cha juu zaidi kurekodiwa ukilinganisha na huduma nyingine kama usafirishaji.
Kwa mujibu wa takwimu za awali zilizotolewa na BoT kupitia ripoti hiyo hifadhi ya fedha za kigeni nchini imefikia Dola za Marekani 5,546.9 sawa na Sh 13.6 bilioni.

BoT imebainisha kuwa kiasi hicho cha fedha kitaiwezesha Tanzania kuagiza bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi kwa miezi minne na nusu ijayo.
Huduma na bidhaa nyingine zilizopaisha hifadhi ya fedha za kigeni nchini Tanzania ni pamoja na mauzo ya dhahabu, tumbaku, mboga mboga, korosho na huduma kama za usafirishaji.
Takwimu Wizara ya Maliasili na Utalii zilizotolewa hivi karibuni zinaonesha kuwa jumla ya watalii wa kimataifa milionin1.2 waliingia nchini kuanzia Januari hadi Julai 2025.
Idadi hiyo ni sawa na ongezeko la asilimia 9.2 ukilinganisha na idaid w=ya watalii wao waliongia nchini kipindi kama hicho mwaka 2024.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk Hassan Abbasi ameinisha kuwa kuwa mafanikio ya sekta hiyo yamechangiwa na mikakati madhubuti ya kuitangaza Tanzania kimataifa kwa kutumia majukwaa mbalimbali.
“Ni wazi kabisa kuwa mafanikio haya yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na ushiriki wa viongozi wakuu wa nchi, usimamizi thabiti wa wizara pamoja na mchango wa wadau mbalimbali waliojitokeza kuitangaza Tanzania katika maonesho ya kimataifa,” amesema Dk Abbas kupitia chapisho la Instagram lililotolewa Septemba 15, 2025.
Latest



