TRC kuajiri wafanyakazi 2460 ujenzi wa SGR Dar- Makutupora

August 20, 2025 2:59 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Ajira hizo zitatolewa kwa awamu mwaka wa fedha 2024/25 na 2025/26.

Arusha. Shirika la Reli Tanzania (TRC) limesema linatarajia kuajiri wafanyakazi 2,460 katika mradi wa reli ya kiwango cha kimataifa (SGR) kwa vipande viwili vya Kutoka Dar es Salaam mpaka Makutopora.

Kwa mujibu wa chapisho la TRC lililotolewa leo Agosti 20, 2025 ajira hizo zitatolewa kwa awamu mwaka wa fedha 2024/25 iliyokwisha muda wake na 2025/26.

“Katika ajira hizo 2,460 utekekezaji wake ni awamu ambapo katika mwaka wa fedha 2024/25 zaidi ya watumishi 500 wameshaajiriwa na mwaka huu wa fedha 2025/26 matarajio ni kuajiri watumishi 272 na TRC itaendelea kuajiri kufikia watumishi 2,460,” imesema taarifa hiyo ya TRC iliyochapishwa katika mtandao wa Instagram.

Aidha, TRC imebainisha kuwa wakati utekekezaji wa utoaji ajira rasmi ukiendelea, tayari ajira 115,000 kutoka kwa  mkandarasi zimenufaisha makundi mbalimbali ikiwemo  vijana wa elimu ya darasa la saba na viwango vingine vya elimu katika fani mbalimbali.

Kati ya hizo  ajira 35,000 ni za moja kwa moja na zaidi ya ajira  80,000 ni zisizo za moja kwa moja zikijumuisha makundi mbalimbali kama baba na mama lishe, bodaboda, bajaji na watoa huduma za makampuni mbalimbali ya mawasiliano kama vocha na laini za simu.

Utoaji wa ajira hizo ni utekelezaji wa maagizo na maelekezo ya Serikali yaliyotaka miradi yote inayoendelea nchini inufaishe wazawa hususani wakazi wa maeneo yanayozunguka miradi.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
17 Oct, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
17 Oct, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
17 Oct, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
HELSB yatoa majina wanufaika wa mkopo awamu ya kwanza

HELSB yatoa majina wanufaika wa mkopo awamu ya kwanza

Nukta TV

TBS yatoa tahadhari matumizi ya ‘sponge’ kupika chapati

TBS yatoa tahadhari matumizi ya ‘sponge’ kupika chapati

Nukta TV

BoT yauza tani 5 za dhahabu kuongeza fedha za kigeni

BoT yauza tani 5 za dhahabu kuongeza fedha za kigeni

Nukta TV