Viwango vya kubadili fedha za kigeni leo Januari 3, 2025

January 3, 2025 11:11 am · Davis Matambo
Share
Tweet
Copy Link

Dar es Salaam. Kuna ongezeko la viwango vya kubadilisha fedha za kigeni na bei ya dhahabu katika soko la Tanzania kati ya jana na leo.

kwa mujibu wa Benki Kuu, thamani ya Dola ya Marekani imepanda kwa Sh10 kwa bei ya kununulia huku bei ya kuuza imepanda mara mbili kwa Tsh20, ongezeko hili linaonyesha kuwa dola imeanza kuwa ghali na huenda kukasababisha shinikizo la mfumuko wa bei.

Wafanyabiashara wanaotegemea kuagiza bidhaa kutoka nje kwa kutumia sarafu hiyo wanaweza kuweka mipango ya kupunguza gharama kwa kuanza mipango ya manunuzi mapema kabla bai haijapanda zaidi.

Bei ya kununua Pauni ya Uingereza (GBP) imeshuka kwa Sh51 lakini bei ya kuuza imepanda kwa Sh314, kulinganisha na jana. Kushuka kwa bei ya kununua kunaweza kuleta fursa kwa wale wanaotaka kuwekeza, wanaopanga safari za nje au kulipa ada za masomo.

Yuan ya China (CNY) imeongezeka sawa kwa Sh3 kwenye bei ya kununua na kuuza, kwa wafanyabiashara wanaofanya manunuzi kwenya soko la China wanapaswa kuzingatia bajeti yao kwa kuwa gharama za biashara zinaweza kuongezeka.

Upande wa dhahabu kuna ongezeko la Sh131,079 kwenye bai ya kununua na Sh132,109 kwa kuuza. kupanda huku huenda kukawa ni fursa nzuri kwa wawekezaji kutazama dhahabu kama njia ya kuhifadhi thamani ya fedha zao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Enable Notifications OK No thanks