Serikali yatangaza ajira 3,633 za walimu masomo ya Biashara yakipewa kipaumbele

December 14, 2024 12:17 pm · Esau Ng'umbi
Share
Tweet
Copy Link
  • Wengine ni wa masomo ya Ushonaji, Uashi, Umeme, Ufundi magari, Uchomeleaji na Utengenezaji Vyuma, Sanaa.
  • Huenda uamuzi huo ukachochea ufaulu wa masomo ya Biashara.

Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania imetangaza ajira 3,633 za walimu wa masomo mbalimbali ikiwemo ya Biashara, Ushonaji, Uashi, Umeme, Ufundi magari, Uchomeleaji na Utengenezaji Vyuma, Sanaa, Useremala, pamoja na Afya ya Wanyama.

Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Desemba 13, 2024 kwa niaba ya Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa imekaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 3,633.

Hata hivyo, Kwa mujibu wa taarifa hiyo yenye Kumb.Na.JA.9/259/01/B/109 zaidi ya asilimia 94 ya nafasi zilizotangazwa ni za walimu wa masomo ya Biashara wakiwa na nafasi 3,425.

Aidha, vigezo na sifa za muombaji vimeainishwa katika kila nafasi ambapo si lazima muombaje awe amehitimu chuo ngazi ya stashahada au shahada katika kada ya ualimu pekee hususan katika masomo ya ufundi kama Ushonaji, Uashi, Umeme, Ufundi magari, Uchomeleaji na Utengenezaji Vyuma.

Itakumbukwa, Novemba 23, mwaka huu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Adolph Mkenda alidokeza kuwa Serikali ipo mbioni kutoa kibali cha ajira 4,000 za walimu wa masomo ya biashara.

Chambuzi za matokeo ya kidato cha nne na cha pili ziliofanywa na Nukta Habari zilibaini kuna upungufu mkubwa wa vitabu pamoja na walimu wa masomo ya biashara jambo ambalo huenda imekuwa sababu ya wanafunzi kutofanya vizuri kwenye masomo hayo.

Huenda uamuzi huo wa Serikali kutoa ajira nyingi kwa walimu wa masomo ya biashara ukachochea kwa kiasi ufaulu wa masomo hayo muhimu katika kutengeneza wataalamu wa uchumi.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Nukta TV

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

Nukta TV

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Nukta TV