Prof. Kindiki aapishwa rasmi kuwa naibu Rais Kenya
- Ni baada ya kupita siku 13 tangu kuteiuliwa kwake.
Arusha. Hatimaye Profesa Kithure Kindiki ameapishwa rasmi kuwa naibu rais wa Kenya ikiwa ni siku 13 tangu kuteuliwa na Rais wa nchi hiyo akichukua nafasi ya Rigathi Gachagua ambaye Bunge la Seneti lilimpigia kura ya kumuondoa madarakani.
Profesa Kindiki aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Utawala wa Kitaifa aliteuliwa Oktoba 18, 2024 na Rais wa Kenya William Ruto na JIna lake kusomwa na Spika wa Moses Wetangula katika kikao kilichokuwa kinaendelea.
Baada ya mchakato wa kuidhinishwa na Bunge kukamilika leo Novemba Mosi,, 2024 kiongozi huyo amepishwa kuwa naibu katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kenyatta (KICC) jijini Nairobi
Akizungumza baada ya kuapishwa amesema hachukulii fiursa hiyo kirahisi hivyo ameahidi kujitolea mkono kumuunga mkono na kuisaidia Serikali hiyo kwa kushirikiana na viongozi wenzake.
“Naahidi kuwa nitakuwa mwaminifu na mwenye uaminifu. Nitajitahidi kwa uwezo wangu wote kufanya kazi kwa bidii pamoja na wenzangu kupunguza mzigo unaoubeba mabegani mwako…
…Nafikiri leo kwangu ni siku ya kupokea heshima kuu zaidi maishani mwangu, na siichukulii kirahisi. Ninamuomba Mungu anipe hekima ya kufanya kinachopaswa kufanywa,”amesema Prof Kindiki.
Kwa upande wake Rais wa nchi hiyo, William Ruto amesema anayo furaha kubwa kushuhudia kuapishwa kwa Prof kindiki kama Naibu Rais wa tatu wa Jamhuri ya Kenya chini ya Katiba ya mwaka 2010 huku akisistiza kumjua kama mtumishi mwaminifu.
“Namjua kama mtumishi mwaminifu wa umma ambaye ana ari na uzalendo wa kipekee kwa taifa letu. Kwa miaka ishirini iliyopita, nimepata heshima ya kushuhudia juhudi za Profesa Kiki kama mwalimu, mwanasheria, kiongozi wa Seneti…
…Na hivi karibuni kama waziri wa serikali.Katika nyadhifa zote hizi, amekuwa na sifa za utendaji bora, maarifa ya hali ya juu, na uadilifu usiotetereka,” amesema Rais Ruto.
Kindiki ameapishwahii leo licha ya kesi inayoendelea mahakamani kupinga kuvuliwa madaraka kwa naibu rais wa awali, Righati Gachagua.
Kiongozi huyo anaingia madarakani wakati ambapo kuna matukio mengi ya watu kukamatwa kiholea na wengine kutoweka nchini Kenya pamoja na nchi hiyo kukabiliwa na hali ngumu ya kiuchumi.