Rais Samia kuchaguliwa Uenyekiti Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC

August 15, 2024 11:36 am · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Atarithi nafasi ya Hakainde Hichilema anayemaliza muda wake.
  • Ni katika Mkutano wa 44 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa (SADC)

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajia kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC akipokea kutoka kwa Rais wa Zambia Hakainde Hichilema anayemaliza muda wake.

Jukumu kubwa la asasi hiyo ni kuangalia masuala yote yanahusiana na Siasa, ulinzi na usalama katika ukanda wa SADC huku changamoto kubwa kwa sasa ikiwa ni namna ya kutafuta suluhu ya kudumu hususani katika eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu Rais Samia atachaguliwa kushika nafasi hiyo katika Mkutano wa 44 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa (SADC) utakaofanyika Agosti 17,2024 mjini Harare nchini Zimbabwe.

Utaratibu wa kuwa Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi, na Usalama ya SADC unafuata mzunguko wa uongozi kati ya nchi wanachama.

Uongozi wa asasi hii huhamishwa kutoka kwa kiongozi mmoja kwenda kwa mwingine kutoka nchi tofauti ili kuhakikisha usawa wa uwakilishi na ushiriki wa nchi wanachama wote katika kusimamia masuala ya siasa na usalama.

Aidha, kwa mujibu wa taarifa hiyo Rais Samia anatarajia kuondoka nchini leo Agosti 15, 2024 kuhudhuria mkutano huo wenye kauli mbinu ya kukuza ubunifu ili kufungua fursa za ukuaji wa uchumi na maendeleo endelevu kuelekea SADC yenye viwanda.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Oct, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Oct, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
WORD BANK: Tanzania haina upungufu wa ajira, changamoto tija yake

WORD BANK: Tanzania haina upungufu wa ajira, changamoto tija yake

Nukta TV

CEOs kung'oka baada ya miaka 10, BoT yarudisha mjadala

CEOs kung'oka baada ya miaka 10, BoT yarudisha mjadala

Nukta TV

Onyo la wachumi ikiwa ukomo wa miaka 10 hautoondolewa kwa CEOs wa benki

Onyo la wachumi ikiwa ukomo wa miaka 10 hautoondolewa kwa CEOs wa benki

Nukta TV