Jengo la Ruwasa Dodoma lageuzwa kuwa makao makuu Jeshi la Polisi

November 22, 2019 8:27 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Jengo hilo lilipo jijini Dodoma la ghorofa nne  lilikuwa la Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA).
  • Rais Magufuli amelitoa kama zawadi, baada ya jeshi hilo kuhamia Dodoma. 
  • Kuhamia Dodoma, kwamnusuru IGP Sirro kutumbuliwa. 

Dar es Salaam. Rais John Magufuli ametoa zawadi ya jengo la ghorofa nne lililokuwa likitumiwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) jijini Dodoma kuwa makao makuu ya Jeshi la Polisi Tanzania. 

Dk Magufuli ametoa zawadi hiyo leo (Novemba 22, 2019) wakati akiweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa nyumba 118 za askari polisi katika eneo la Nzuguni, jijini humo.

“Nimeamua kuwapa jengo moja kubwa, lenye ghorofa nne. Jengo hilo lilikuwa linatumiwa na Ruwasa, sasa ndiyo yatakuwa makao makuu ya Jeshi la Polisi,” amesema Rais.

Rais ametoa zawadi hiyo, baada ya jeshi hilo kutimiza azma ya Serikali ya kuhamia Dodoma kama zilivyofanya ofisi nyingine za Serikali akiwemo Rais Magufuli mwenyewe ambaye alihamia rasmi hivi karibuni.

“Lakini kwa sababu mmehamia hapa, nakushukuru! na kwa sababu askari hasubiri nyumba, nimeamua kuwapa zawadi moja. Siyo hela, mimi sitoagi hela,” amesema Rais Magufuli. 

Awali makao makuu ya jeshi hilo yalikuwa kwenye ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani jijini Dar es Salaam. 


Soma zaidi: 


Hata hivyo, hatua hiyo ya kuhamia Dodoma kwa Jeshi la Polisi, imemnusuru Mkuu wa jeshi hilo, IGP Simon Sirro kuondolewa katika nafasi yake, baada ya Rais kueleza kuwa angekuwa hajahamia, angemteua mtu mwingine. 

“Nimefurahi ulivyoeleza kwamba mmehamia hapa, na wewe IGP (Simon Sirro) umehamia hapa ningekushangaa kuona mimi nimehamia wewe bado uko, ningeteua IGP wangu wa hapa Dodoma,” amesema Rais.

Amelitaka jeshi hilo kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi na weledi katika kulinda raia na mali zao na kuhakikisha nchi inakuwa na amani na usalama wakati wote ili kuendeleza biashara na kuvutia wawekezaji.

Akizungumza katika uzinduzi huo, IGP Sirro amesema nyumba hizo za polisi zinajengwa kwa nguvu kazi (force account) na zitakamilika Desemba 31, 2019. 

Magufuli ameweka wazi kuwa nyumba hizo zitasaidia kupunguza uhaba wa nyumba za askari polisi nchini na kuwaongezea ufanisi wa kutekeleza majukumu yao ya kila siku. 

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Nukta TV

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Nukta TV

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Nukta TV