Tanzania kuunganisha mifumo ya uwekezaji kielektroniki

May 27, 2021 10:56 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Imeanza kufanya maboresho ya huduma za uwekezaji  kwa kuunganisha mifumo ya kielektroniki kwa taasisi na idara 11 za Serikali.
  • Itasaidia kurahisisha utoaji wa vibali na leseni za uwekezaji nchini.

Dar es Salaam. Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimeanza kufanya maboresho ya huduma za uwekezaji  kwa kuunganisha mifumo ya kielektroniki kwa taasisi na idara 11 za Serikali zinazotoa huduma kwenye kituo cha pamoja cha uwekezaji.

Maboresho hayo yatasaidia kurahisisha utoaji wa vibali na leseni za uwekezaji kwa kuunganisha mifumo hiyo ili kuwa na dirisha moja la uwekezaji nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Dk Maduhu Kazi amesema maboresho hayo yatasaidia kuongeza ufanisi katika kutoa huduma kwa wawekezaji na kuimarisha utendaji kazi wa kituo hicho.

“Kama mnavyofahamu, Mheshimiwa Rais (Samia Suluhu Hassan) alitoa maelekezo ya namna ya kuboresha huduma za uwekezaji, kikao hiki ni muendelezo wa utekelezaji wa majukumu hayo, tulishaanza kuyafanyia kazi, na sasa tunaendelea, lengo ni kutoa huduma bora zaidi za uwekezaji” amesema Dk Kazi.

Dkt Maduhu amefanya kikao cha pamoja na  wakuu wa taasisi na idara za Serikali 11 zinazotoa huduma kwenye kituo cha huduma kwa wawekezaji cha pamoja (One Stop Facilitaion Centre) na kubainisha kuwa mchakato wa maboresho hayo unaendelea kufanyiwa kazi.


Zinazohusiana: 


Dk Kazi amepokea taarifa ya hatua ambazo zimechukuliwa kwa kila taasisi na idara husika zikiwepo kila taasisi kufungua mfumo wa kielektroniki kwa ajili ya utoaji vibali na leseni mbalimbali.

Maboresho haya yanaelezwa kuwa yatawawezesha wawekezaji wanaowekeza nchini kupata huduma kwa muda mfupi na kwa kutumia gharama ndogo.

Baadhi ya Taasisi zilizoshiriki katika kikao hicho ni pamoja na Uhamiaji, Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA), Mamlaka ya Chakula na Dawa (TMDA), Mamlaka ya Mapato Tanzani (TRA), Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira  (NEMC), Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi).

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Nukta TV

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

Nukta TV

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Nukta TV