Jaji mstaafu Othman ateuliwa kuwa mkuu wa chuo Ardhi

August 17, 2021 12:12 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Aliwahi kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania
  • Pia Rais Samia amemteua Profesa Elisante Ole Gabriel kuwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania. 

Dar es Salaam. Rais Samia Suluh Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali akiwemo Jaji Mkuu mstaafu Mohamed Chande Othman ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU).

Jaji Othman amechukua nafasi iliyoachwa na Waziri Mkuu wa zamani na Makamu wa Rais wa Tanzania, Cleopa Msuya. 

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Jaffar Haniu katika taarifa yake iliyotolewa leo Agosti 17, 2021 amesema Rais Samia pia amemteua Profesa Elisante Ole Gabriel kuwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania. 

Kabla ya uteuzi huu Profesa Ole Gabriel alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi upande wa mifugo. Profesa Ole Gabriel anachukua nafasi ya Mathias Kabunduguru ambaye amestaafu.

Profesa Ole Gabriel ataapishwa Agosti 21, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam pamoja na mabalozi wateule watatu ambao ni Balozi mteule Luteni Jenerali Yakub Hassan Mohamed aliyeteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Uturuki.

Balozi mteule Mahmoud Thabit Kombo aliyeteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia na Balozi Mteule Elsie Sia Kanza aliyeteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
7 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
7 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV