Tahadhari ongezeko la watu duniani
- Hadi Novemba mwaka huu, dunia itakuwa na watu bilioni 8.
- Wadau washauri kujiandaa dhidi ya ongezeko hilo.
Dar es Salaam. Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) limeitaka dunia kuchukua hatua za kufanya uwekezaji wenye busara na kuongeza ubunifu ili kukabiliana na athari za ongezeko la watu.
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa (UN) idadi ya watu duniani inayokadiriwa kufikia bilioni 8 mwishoni mwa mwaka 2022.
Pia imetangaza kuwa mwaka 2023 India inakadiriwa kuwa nchi yenye watu wengi zaidi, kuipita China.
UN imeweka wazi kuwa zaidi ya nusu ya matarajio ya ongezeko la idadi ya watu duniani hadi mwaka 2050 yatakuwa katika nchi nane ambazo ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Misri, Ethiopia, India, Nigeria, Pakistani, Ufilipino na Tanzania.
“Nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara zinatarajiwa kuchangia zaidi ya nusu ya ongezeko la watu linalotarajiwa linalotarajiwa kufikia mwaka 2050,” imeeleza taarifa ya UN.
UNFPA imesema takwimu hizi mpya zimekuja wakati dunia ikiendelea kupambana na janga linaloendelea la Uviko-19 ambalo limeua zaidi ya watu milioni 6 duniani kote.
Baada ya kutolewa kwa taarifa hiyo, UNFPA liliwahoji watu mbalimbali kupata maoni yao hasa wanahusika moja kwa moja na idadi ya watu.
Soma zaidi:
Mkurugenzi Mtendaji wa UNFPA Dk Natalia Kanem kuhusu ongezeko la watu amesema “Watu ndiyo suluhisho, si tatizo. Nambari ni muhimu, lakini hebu tuhesabu kwa uangalifu. Ulimwengu wenye ustahimilivu wa bilioni 8, ulimwengu unaozingatia haki na chaguzi za mtu binafsi, unatoa uwezekano usio na kikomo – uwezekano wa watu, jamii na sayari yetu ya pamoja kustawi na kustawi.”
Maoni ya taarifa hii yaongezeko la watu pia yamepokelewa kwa muitikio tofauti hususan mashariki ya mbali ambapo kumekuwa kukishuhudiwa vita na changamoto mbalimbali.
Abdulrahman Al-Ward (26), mwanaharakati wa vijana nchini Yemen, akihojiwa na UNFPA mbali na nchi yake kukumbwa na vita visivyokoma amesema, “pamoja na wazimu unaoendelea ulimwenguni, watu wengi zaidi inamaanisha mateso zaidi.”
Anton Massouh (24), mhandishi kutoka Homs nchini Syria yeye ingawa nchi yake ipo kwenye mzozo mbaya wa muda mrefu ana matumaini chanya.
“Ulimwengu unaofikia idadi hii utamaanisha sayansi zaidi, uvumbuzi na ugunduzi. Ukuaji huu utachochea teknolojia na utafiti zaidi,” amesema Al-Ward.
Suala la uwekezaji limebuka kutoka kwenye mataifa mbalimbali ambapo kuna wasiwasi mkubwa juu ya kutokea kwa majanga, uharibifu wa mazingira na usalama mdogo wa binadamu kama anavyoeleza Ibtihal Ait Layachi mkunga katika hospitali ya izazi ya Tetouan nchini Morocco
“Kukabiliana na majanga ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya tabianchi, uharibifu wa maliasili, magonjwa ya mlipuko na vita, anaamini kwamba mustakabali wa maisha uko hatarini,” amesema Layachi.
Latest