CHATI YA SIKU: Uzalishaji wa maziwa waongezeka Tanzania lakini mwenendo wa unywaji hauridhishi

November 16, 2018 11:42 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Kwa wastani mtu mmoja anakunywa lita 47 za maziwa kwa mwaka ikiwa ni pungufu zaidi ya mara nne ya kiwango kinachopendekezwa na FAO cha lita 200 kwa mwaka
  • Uzalishaji na usindikaji maziwa wazidi kuongezeka nchini lakini bado kuna fursa zaidi kutoka katika sekta hiyo.

Dar es Salaam. Licha ya uzalishaji na usindikaji wa maziwa kuongezeka nchini bado mwenendo wa unywaji wa maziwa kwa mwananchi mmoja mmoja siyo wa kuridhisha.

Kwa wastani mtu mmoja anakunywa lita 47 za maziwa kwa mwaka ikiwa ni pungufu mara nne ya kiwango kinachopendekezwa na Shirika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO) kwa mtu mmoja kunywa lita 200 kwa mwaka.

Hii ndiyo hali halisi kwa takwimu chache za hivi karibuni kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi

Enable Notifications OK No thanks