Utambulisho, uwekezaji kuzibeba ‘Startups’ Tanzania

February 7, 2019 7:44 pm · Zahara
Share
Tweet
Copy Link
  • Washauriwa kujisajili na kuwavutia wawekezaji waweze kuwekeza katika biashara zao.
  • Washauriwa kujitokeza katika makongamano mbalimbali kuhusu wajasiriamali ili kujifungulia milango ya kufahamiana na watu na kujifunza.

Dar es Salaam. Wadau wa masuala ya teknolojia wamezishauri kampuni zinazochipukia (Startups) kusajili kampuni zao ili zitambulike rasmi na kuvutia wawekezaji kuwekeza mitaji yao.

Ushauri huo umekuja kutokana na kuwepo kwa vijana wabunifu wenye mawazo ujasiriamali katika teknolojia lakini hawapo katika mfumo rasmi wa kuendeleza shughuli zao.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Sahara Ventures, Jumanne Mtambalike aliyekuwa akizungumza leo (Februari 7, 2019) jijini hapa wakati wa utiaji saini wa makubaliano na kampuni ya Chanzo Capital ya Ghana kuandaa kongamano la wabunifu la ‘Sahara Sparks’, amesema ni wakati kwa vijana wabunifu kuyafanyia kazi mawazo yao ili wapate fursa za kukuza mitaji ya biashara.

“Kwenye hili kongamano watapatikana wawekezaji sasa hawatakuwa na muda wa wazo lako watataka biashara ambayo ipo kabisa na inajiendesha yenyewe,” amesema.

 MAKUBALIANO: Pichani kushoto ni Erick Osiakwan kutoka Chanzo Capital na kulia Jummanne Mtambalike kutoka Sahara Ventures wakisaini mkataba wa kuandaa Kongamano la Sahara Sparks la wabunifu linalotarajiwa kufanyika mwaka huu. Picha|Zahara Tunda.

Mtambalike ambaye amewahi kufanya kazi na kituo cha kuendeleza ubunifu cha Buni Hub amesema vijana wenye nia kukua kibiashara wanatakiwa kujenga mfumo wa kibiashara unaotambulika na mamlaka za usajili nchini.

Pia kuwa na timu ya wataalam waliobeba katika masuala ili kuwa na uwezo wa kuwashawishi wakezaji kuweka mitaji katika kampuni zao.

Kongamano la Sahara Sparks linatarajiwa kufanyika Oktoba 7 hadi 12 mwaka huu jijini hapa likiwa na lengo kuwakutanisha wadau mbalimbali wa nje na ndani ya nchi kutafakari juu ya matumizi ya teknolojia, uvumbuzi na ujasiriamali yanavyogusa uchumi na maendeleo ya Afrika.


Zinazohusiana: 


Sambamba na hilo kampuni hizo zimetakiwa kuwekeza katika matumizi ya teknolojia yanayosaidia kutatua changamoto za jamii.

“Huwa tunaangalia sana wabunifu na wajasiriamali wenye teknolojia ndani yake na vilevile jinsi gani inaweza kuingiza pesa kwa huyo mjasiriamali ili wawekezaji wavutie kuwekeza,” amesema Erick Osiakwan mjasiriamali na mwekezaji kutoka kampuni ya Chanzo Capital.

Enable Notifications OK No thanks