Rais Magufuli awatunuku kamisheni maafisa 146 JWTZ

March 30, 2019 9:55 am · TULINAGWE ALSON
Share
Tweet
Copy Link
  • Waliotunukiwa ni maofisa wanafunzi 146 wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kuwa na cheo cha Luteni Usu Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya kuhitimu mafunzo ya mwaka mmoja.
  • Kati ya maafisa hao wanawake ni sita na wanaume ni 140.

Dar es Salaam. Rais John Magufuli amewatunuku kamisheni maofisa wanafunzi 146 wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kuwa na cheo cha Luteni Usu Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya kuhitimu mafunzo ya mwaka mmoja.

Maafisa hao wametunukiwa ukamishna baada ya kupata mafunzo katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi mkoani Arusha yaliyoanza Machi 12 mwaka 2018.

Waliotunukiwa kamisheni na Rais Magufuli ni maafisa wapya wa JWTZ kundi la 65 kwa mwaka 2019 ambapo jumla yao ni 146, kati yao 140 ni wanaume na sita ni wanawake.


Soma zaidi:


Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi mkoani Arusha, Bregadia Jenerali Steven Mkande amesema  kati ya idadi hiyo ya maafisa waliotunukiwa kamisheni watatu wana shahada ya uzamili, 116 wana shahada ya kwanza na mmoja ana stashahada ya uzamili.

Stashahada ya juu ina maafisa watatu huku madaktari wakiwa 23 kati yao 21 ni madaktari wa kawaida wa binadamu na wawili ni madaktari wa wa kinywa na meno.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali ikiwemo Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan; Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
17 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
17 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Siku ya Familia, Mtoto wa Afrika kuadhimishwa Juni 30, 2026

Siku ya Familia, Mtoto wa Afrika kuadhimishwa Juni 30, 2026

Nukta TV

Wadau wa 'kubet" watoa ya moyoni, pendekezo kupanda kwa tozo 5%

Wadau wa 'kubet" watoa ya moyoni, pendekezo kupanda kwa tozo 5%

Nukta TV

Wasemayo wananchi, vocha za kukwangua kupigwa maruku mijini

Wasemayo wananchi, vocha za kukwangua kupigwa maruku mijini

Nukta TV