Rais Magufuli akataa kuongeza mikoa, wilaya mpya

April 5, 2019 11:30 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link

 Rais John Magufuli amesema amejipanga kuboresha huduma za jamii na siyo kuanzisha mikoa mipya. Picha| Mtandao.


  • Amesema ujenzi wa ofisi za wakuu wa mikoa na wilaya unaongeza gharama za uendeshaji ambazo zingeelekezwa katika uboreshaji wa huduma za kijamii ili kuwanufaisha wananchi.
  • Amesema matakwa ya wananchi ni kuona shida zao zinatatuliwa na sio kuwaona wakuu wa mikoa na wilaya wakitembea barabarani
  • Kwa maoni yake sababu kwa Tanzania kuwa na mikoa 26 badala yake ingekuwa na mikoa michache. 

Dar es Salaam. Rais John Magufuli amesema hana mpango wa kuongeza idadi ya mikoa na wilaya badala yake pesa ambazo zingetumika katika shughuli za utawala zielekezwe katika kuboresha huduma za jamii ili kuboresha maisha ya wananchi. 

Rais Magufuli aliyekuwa akihutubia mkutano wa hadhara wilayani Tunduru mkoa wa Ruvuma leo (Aprili 5, 2019) amesema wananchi hawahitaji ofisi za wakuu wa mikoa na wilaya bali wanahitaji huduma bora za jamii ikiwemo maji, umeme, vituo vya afya.

“Ndiyo maendeleo haya tunayoyahitaji siyo wakuu wa mikoa. Kwa hiyo ninazungumza hapa kwa niaba ya wengine huko na wilaya nyingine zilizo na ugonjwa wa kuanzisha mikoa na wilaya kwangu hapana,” amesema Rais Magufuli.

Amesema ujenzi wa ofisi za Serikali na kuwalipa mishahara watendaji watakaotumia majengo ya ofisi zinazoanzishwa ni gharama kubwa, jambo linalorudisha nyuma mipango ya kuwafikishia wananchi maendeleo. 

Amebainisha kuwa matakwa ya wananchi ni kuona shida zao zinatatuliwa na siyo kuona wakuu wa mikoa na wilaya wakitembea barabarani.

“Ukichukua hela ukaanza kujenga majengo ya wakuu wa mikoa ambao utakuwa unawalipa mshahara halafu usiwapelekee maji, hujaisaidia Tunduru kwa sababu mahitaji ya watu wa Tunduru si kumuona Mkuu wa Mkoa na kitambi chake akitembea barabarani wanataka shida zao wanatunduru zimaliziwe,” amesisitiza Rais. 

Mpaka sasa Tanzania ina mikoa 31 ambapo 26 iko Tanzania bara na mitano iko Zanzibar. 


Soma zaidi:


Katika mkutano huo ambao ni sehemu ya ziara ya Rais ya siku sita mkoani Ruvuma, baadhi ya viongozi walimuomba aipandishe hadhi wilaya ya Tunduru na kuwa mkoa kwa sababu ya ukubwa wake ili kusogeza karibu huduma kwa wananchi.

Hata hivyo, katika maelezo yake Rais Magufuli amesema akitekeleza ombi hilo gharama za uendeshaji Serikali zitaongezeka na wananchi wa Tunduru watakosa huduma ikiwemo barabara ambazo ni muhimu kwa shughuli za uchumi na biashara.

“Unaweza kugawanya Tunduru ukawa na mikoa mitatu humu, hata ukasema Tunduru sasa kila tarafa utakuwa mkoa mtakuwa mnaongeza gharama bure, fedha ambazo zingepelekwa kwa wananchi zinatumika katika masuala ya utawala, ni lazima niwaambie ukweli,” amesema Rais. 

Amesema kwa maoni yake hakukuwa na sababu ya Tanzania bara kuwa na mikoa 26, tungeweza kuwa na mikoa michache na gharama za kuendeshea mikoa hiyo zingetumika kwa maslahi ya wananchi. 

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, inampa mamlaka Rais wa Tanzania uwezo wa kugawa nchi kwa kadiri atakavyoona inafaa. 

Serikali ya awamu ya nne iliyokuwa ikiongozwa na Rais Jakaya Kikwete alifanikiwa kuongeza mikoa minne ya Geita, Katavi, Njombe na Simiyu ukilinganisha na 21 iliyokuwepo awali ambapo mpaka sasa Tanzania ina mikoa 31. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
21 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
21 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
21 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Nukta TV

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Nukta TV

FAHAMU KUHUSU SIKOSELI | Part 1: Ugonjwa wa kurithi, unaotesa maelfu ya watoto Tanzania

FAHAMU KUHUSU SIKOSELI | Part 1: Ugonjwa wa kurithi, unaotesa maelfu ya watoto Tanzania

Nukta TV