Ndege yalipuka Urusi, watu 41 wafariki dunia

May 6, 2019 5:54 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Ndege aina ya Sukhoi Superjet-100 inayomilikiwa na shirika la ndege la Aeroflot la Urusi imewaka moto baada ya kutua kwa dharura katika uwanja wa ndege wa Sheremetyevo katika jiji la Moscow.
  • Ilikuwa na abiria 73 na maafisa watano.

Ndege aina ya Sukhoi Superjet-100 inayomilikiwa na shirika la ndege la Aeroflot la Urusi imewaka moto na kuua watu 41 baada ya kutua kwa dharura katika uwanja wa ndege wa Sheremetyevo katika jiji la Moscow.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Urusi, ndege hiyo ilikuwa na abiria 73 na maafisa watano, ambapo kati ya waliofariki ni watoto wawili na mhudumu mmoja.

Video fupi inayosambaa katika mitandoa ya kijamii inaonyesha baadhi ya abiria wakitumia mlango wa dharura na kutoka kwenye ndege hiyo ya Aeroflot iliyokuwa inateketea moto.

           

Taarifa ya Aeroflot iliyotolewa jana (Mei 5, 2019) imeeleza kuwa ndege hiyo iliondoka uwanja wa ndege wa Sheremetyevo kutoka eneo la Murmansk lakini baada ya kutua kwa dharurua katika uwanja huo, injini za ndege hiyo ziliwaka moto katika njia kuu wa ndege.

Shirika hilo limesema maafisa hao wa ndege walijitahidi kadri ya uwezo wao kuwaokoa abiria lakini wachache walifanikiwa kutolewa katika muda wa sekundi 55 na baadaye ndege ililipuka. 

Maafisa wa vyombo vya dola kwa kushirikiana wanaendelea kuchunguza chanzo cha ndege hiyo kulipuka muda mfupi baada ya kutua kwa dharura katika uwanja Sheremetyvo

Taarifa za kulipuka kwa ndege hiyo tayari zimemfikia Rais wa Urusi Vladimir Putin  ameeleza masikitiko yake kwa familia za waathiriwa. Eneo hilo la Murmansk limetangaza siku tatu za maombolezi.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
21 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
21 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Nukta TV

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Nukta TV

FAHAMU KUHUSU SIKOSELI | Part 1: Ugonjwa wa kurithi, unaotesa maelfu ya watoto Tanzania

FAHAMU KUHUSU SIKOSELI | Part 1: Ugonjwa wa kurithi, unaotesa maelfu ya watoto Tanzania

Nukta TV