Chatbot: Teknolojia inayosaidia ukuaji wa soko la bidhaa

May 16, 2019 1:33 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link

  • Ni programu ya kompyuta iliyotengezwa kwa ajili ya kuwezesha mawasiliano kati ya  binadamu na mashine. 
  • Ni njia rahisi ya kuimarisha mahusiano na wateja, kuboresha huduma na bidhaa. 

Dar es salaam. Katika kuhakikisha kampuni au masharika yanaendelea kuuza bidhaa na kutoa huduma bora kwa wateja, teknolojia imekuwa kiungo muhimu cha kufanikisha mikakati ya kukuza soko.

Moja ya teknolojia hizo ni matumizi ya ‘chatbot’ ambayo imeanza kujipatia umaarufu kwa kampuni zinazohitaji kuimarisha mahusiano na mawasiliano na wateja wake ili kuhakikisha huduma zinapatikana saa 24 hata pasipo kuhitaji msaada wa mtu. 

Chatbot ni programu ya kompyuta iliyotengezwa kwa ajili ya kuwezesha mawasiliano kati ya  binadamu na mashine. 

Programu hiyo imekuwa fursa muhimu kwa ukuaji wa masoko ya kijigitali kwasababu mtu anaweza pata taarifa za masoko  kwa masaa 24 bila ya mwingiliano wa binadamu  kupitia tovuti na programu tumishi mbalimbali.

Ripoti ya Kongamano la masuala ya teknolojia la Gartner iliyotolewa mwaka 2011 inaeleza kuwa ifikapo  mwaka 2020 asilimia 80 ya biashara zitakuwa zinaendeshwa kwa sehemu kubwa na mashine (chatbots), jambo litakalopunguza kazi zinazofanywa na binadamu.


Zinazohusiana:Kutana na shangazi roboti wa Tanzania aliyepania kutokomeza mimba za utotoni


Kutokana na umuhimu wake, taasisi mbalimbali nchini zinatumia teknolojia hiyo ili kurahisisha mawasiliano na utoaji huduma katika maeneo yao. 

Mathalan, benki ya  CRDB kupitia tovuti yake ina huduma inayojulikana kama ‘We are Online Let’s chat’;na benki ya Stanbic (Webchat). 

Chatboat nyigine ni ‘eshangazi’ (shangazi wa kimtandao ) ni teknolojia iliyobuniwa na kampuni ya Index Lab ili kutoa elimu na ushauri kwa vijana kuhusu afya ya uzazi na jinsia ili kupambana na mimba za utotoni kupitia Facebook Messanger.

Shangazi huyo roboti anapatikana kupitia Facebook Messenger kwa wale wanaomiliki simu janja (smartphones) na hujibu maswali papo kwa papo. Picha|eshangazi

Ingawa chatboat ya kwanza ilitengenezwa mwaka 1950 na mtaalamu wa kompyuta kutoka Uingereza, Alan Turing lakini ilianza kutumika zaidi mwaka  2014 na kuleta mapinduzi ya teknolojia ya mawasiliano duniani. 

 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
25 Sep, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
25 Sep, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Ukweli kuhusu Mama Fatma Karume, mwanamke aliyeshika kiganja cha historia ya Zanzibar

Ukweli kuhusu Mama Fatma Karume, mwanamke aliyeshika kiganja cha historia ya Zanzibar

Nukta TV

Tanzania yasisitiza amani na suluhu Mashariki ya Kati, kikao cha 81 cha UN

Tanzania yasisitiza amani na suluhu Mashariki ya Kati, kikao cha 81 cha UN

Nukta TV

Rais Mwinyi: Wananchi wanataka viongozi walete maendeleo, si malumbano ya kisiasa

Rais Mwinyi: Wananchi wanataka viongozi walete maendeleo, si malumbano ya kisiasa

Nukta TV