Majaliwa awakaribisha wawekezaji wa Rwanda kuwekeza katika kilimo, viwanda

June 11, 2019 12:31 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Spika wa Bunge la Rwanda, Donatile Mukabalisa, ofisini kwa Waziri Mkuu, Bungeni jijini Dodoma, Juni 11.2019. Picha| Ofisi ya Waziri Mkuu.


Serikali ipo tayari kuwapokea na kuwapa ushirikiano wawekezaji kutoka katika nchi hiyo ili waje kuwekeza katika sekta mbalimbali zikiwemo za viwanda, kilimo, madini na utalii.

  • Bandari ya Dar es Salaam na ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) utarajiwa kusaidia katika usafirishaji wa mizigo kwenda hadi nchini Rwanda.

Dar es Salaam. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewakaribisha wawekezaji kutoka nchini Rwanda waje wawekeze katika sekta mbalimbali zikiwemo za viwanda, kilimo, madini na utalii na kuwa Serikali itawapa ushirikiano wa kutosha.

Ameyasema hayo leo leo (Juni 11, 2019) alipokutana na kufanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Rwanda, Donatille Mukabalisa, Ofisini kwake Bungeni jijini Dodoma.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu leo, Serikali ipo tayari kuwapokea na kuwapa ushirikiano wawekezaji kutoka katika nchi hiyo ili waje kuwekeza katika sekta mbalimbali zikiwemo za viwanda, kilimo, madini na utalii.

Waziri Mkuu amesema Tanzania na Rwanda ni nchi zenye uhusiano mzuri, hivyo amemwakikishia Spika Donatille kwamba Serikali itauimarisha uhusiano huo.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema Serikali inatekeleza mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) ambao utarajiwa kusaidia katika usafirishaji wa mizigo kwenda hadi nchini Rwanda.


Soma zaidi: 


Naye, Spika Donatille ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano mkubwa inaoutoa kwa Serikali ya Rwanda na kumuhakikishia Waziri Mkuu kwamba watauendeleza.

Spika huyo amesema ushirikiano wa Tanzania na Rwanda ni muhimu katika uchumi kwa kuwa wanatumia bandari ya Dar es Salaam katika kusafirisha asilimia kubwa ya mizigo yao.

Wananchi wa nchi hizo mbili nao wametakiwa wawe na ushirikiano katika nyanja mbalimbali kama za kibiashara ambapo Spika huyo naye ametumia fursa hiyo kuwakaribisha Watanzania wakawekeze nchini Rwanda. 

Enable Notifications OK No thanks