Gmail kuja na mabadiliko makubwa mwanzoni mwa Julai 2019

June 12, 2019 8:34 am · Daniel
Share
Tweet
Copy Link
  • Katika maboresho hayo, kutakuwa na huduma ya kukubali au kukataa wito kwenye tukio, kujaza maswali, kujibu maoni, na orodha za kuvinjari(browsing catalogs).
  • Maoni ya kwenye Google Docs sasa yatakuja  moja kwa moja kwenye barua pepe ya mtumiaji ili aweze kujibu maoni hayo kwa haraka.

Dar es Salaam. Mwanzoni mwa mwezi ujao huduma ya barua pepe ya Google (gmail) itafanyiwa maboresho kwa kuongezewa kipengele  kinachoitwa ‘dynamic email’  ikiwa ni moja ya mabadiliko makubwa ambayo Google imeyafanya baada ya yale ya mwaka jana ya kalenda na sehemu ya notebook (task bar) ambayo yalimfanya mtumiaji asiishie kutuma na kupokea baruapepe tu.

Mabadiliko hayo makubwa kwenye gmail, ambayo yalianza kupatikana kwa majaribio (beta version) tangu Machi mwaka huu kwa wateja wa biashara, sasa yataanza kutumika rasmi kuanzia Julai 2.

Katika maboresho hayo, mtumiaji wa barua pepe ataweza kuifanya isibadilike kwenye akaunti zake zote  (default on all Gmail accounts) huku akiweza kufanya kazi kadhaa akiwa ndani ya barua pepe yake bila kuondoka na kwenda kwenye ukurasa mwingine.


Zinazohusiana:Miaka 15 ya Gmail inavyoongeza thamani bidhaa za Google

                           Nukta Africa yateuliwa katika mpango wa Google


Pia kwenye barua pepe kutakuwa na huduma ya kukubali ama kukataa mwaliko wa tukio maarufu kwa Kiiengereza RSVP-ing , kujaza maswali, kujibu maoni, na orodha za kuvinjari(browsing catalogs).

Itakavyofanya kazi

Badala ya kupokea ujumbe pale mtu apokutaja kwenye maoni  yaliyoandikwa kwenye nyaraka za programu ya kuandika Google Docs), katika mabadiliko mapya maoni hayo yatakuja kwenye barua pepe yako ya gmail na utaweza kujibu kirahisi na kwa haraka.

Pindi huduma hiyo itakapo anza kampuni ambazo zitaweza kutumia pia ni Booking.com, Despegar, Doodle, Ecwid, Freshworks, Nexxt, OYO Rooms, Pinterest, na RedBus, huku Google ikieleza huo sio mwisho wa idadi ya watumiaji na kusisitiza huduma hiyo kwa siku za mbeleni itakuwa kwa watumiaji wote.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
21 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
21 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Nukta TV

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Nukta TV

FAHAMU KUHUSU SIKOSELI | Part 1: Ugonjwa wa kurithi, unaotesa maelfu ya watoto Tanzania

FAHAMU KUHUSU SIKOSELI | Part 1: Ugonjwa wa kurithi, unaotesa maelfu ya watoto Tanzania

Nukta TV