Samaki wabichi, nyumba za kulala wageni vyachangia kupaisha mfumuko wa bei

July 8, 2019 2:30 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • NBS yaeleza kuwa mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia Juni 2019 ulipaa hadi asilimia 3.7 kutoka 3.5 ya Mei mwaka huu.

Dar es Salaam. Kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia Juni mwaka huu imepaa hadi asilimia 3.7 kutoka asilimia 3.5 iliyorekodiwa Mei 2019 ikichagizwa zaidi na kuongezeka kwa bei za bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula zikiwemo dagaa, samaki wabichi na mafuta.

Takwimu mpya za mfumuko wa bei zilizotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) leo (9 Julai 8, 2019) zinabainisha kuwa baadhi ya bidhaa za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa mfumuko wa bei ni pamoja na samaki wabichi kwa asilimia 27.3, unga wa mahindi (asilimia 3.6), unga wa ngano (asilimia 4.4), mtama (asilimia 4.9) na dagaa kwa asilimia 16.5.

Bidhaa hizo ni moja ya vyakula vikuu vinavyotumika zaidi nchini kwa familia za vipato vyote.

“Kwa upande mwingine baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa mfumuko wa bei wa Juni 2019 ni pamoja na dizeli kwa asilimia 11.4, petroli (asilimia 4.9), gharama za kulala kwenye nyumba za wageni (5.8) na vitabu vya shule kwa asilimia 2.4,” imeeleza taarifa ya NBS kwa vyombo vya habari.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
26 Sep, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
26 Sep, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
26 Sep, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Lissu: Serikali haikutishwa, hivyo hakuna kosa la uhaini

Lissu: Serikali haikutishwa, hivyo hakuna kosa la uhaini

Nukta TV

Ratiba rasmi mitihani ya darasa la nne, saba na kidato cha pili na nne 2026.

Ratiba rasmi mitihani ya darasa la nne, saba na kidato cha pili na nne 2026.

Nukta TV

Wanu ataja changamoto sita, ratiba ya mitihani ya taifa yabadilika

Wanu ataja changamoto sita, ratiba ya mitihani ya taifa yabadilika

Nukta TV