Ufaulu kidato cha sita waongezeka kwa asilimia 0.74

July 11, 2019 10:44 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Ufaulu umeongezeka kutoka asilimia 97.58 mwaka 2018  hadi  asilimia 98.32  mwaka huu.

Dar es Salaam. Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha sita ya mwaka 2019 huku ufaulu ukiongezeka kwa asilimia 0.74 ukilinganishwa na mwaka jana. 

Akitangaza matokeo hayo leo (Julai 11, 2019) Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde amesema ufaulu umeongezeka kutoka asilimia 97.58 mwaka 2018  hadi  asilimia 98.32  mwaka huu.

Katika matokeo ya mitihani hiyo iliyofanyika Mei 6 hadi 23 mwaka 2019, watahiniwa 91,236 walisajiliwa kufanya mitihani wakiwamo wanawake 31,948 sawa na asilimia 41.56 huku wavulana wakiwa 53,350 sawa na asilimia 58.44.

Dk Msonde amesema wanafunzi 90,0001 walifanya mtihani kati ya wanafunzi 91,236 waliosajiliwa ambao ni sawa na asilimia 98.85. 

Matokeo ya kidato cha sita >>>>>>>> bonyeza hapa 

Enable Notifications OK No thanks