Instagram yafanya majaribio ya kuficha idadi ya “likes” na “views” za watumiaji wake
- Lengo la majaribio hayo ni kuwawezesha wafuasi wa akaunti za Instagram kuweka mawazo yao kwenye picha na video na siyo idadi ya likes au views alizopata mtu.
- Yasema imezingatia maslahi mapana ya watumiaji wake.
Mtandao wa instagram unafanya majaribio katika nchi saba duniani ili kuzuia watu kuona idadi ya watu waliopenda (likes) na waliotazama (Views) picha na video ambazo zinawekwa kwenye mtandao huo.
Lengo la majaribio hayo ni kuwawezesha wafuasi wa akaunti za Instagram kuweka mawazo yao kwenye picha na video na siyo idadi ya likes au views alizopata mtu.
Majaribio hayo yanafanyika katika nchi za Australia, Brazil, Canada, Ireland, italia, Japan na New Zealand ambapo mtandao huo utaficha ‘likes’ na ‘views’ ambazo zimekuwa zikionekana chini ya video au picha iliyowekwa Instagram.
Hata hivyo, mtu aliyeweka video au picha ataendelea kuona idadi ya watu walio like au kuangalia video yake.
Majaribio hayo ambayo sasa yamenza kufanyika nchini Canada ambapo watu wanao like picha au kuangalia video katika mtandao huo wenye watumiaji zaidi ya bilioni 1.2 sasa hawataweza kuziona badala yake wataona picha, video na ujumbe uliowekwa.
Zinazohusiana: Instagram yaja na mbinu mpya kudhibiti uzalilishaji mtandaoni
Mkuu wa Instagram, Adam Mosseri katika mahojiano yake ya hivi karibuni na shirika la habari la CBS News amesema wamefanya majaribio hayo kwa ajili ya maslahi mapana ya watumiaji wake.
“Hatutaki Instagram iwe na ushindani. Tunaka Iwe sehemu ambayo watu watatumia nguvu zao kwa ajili ya kujuana na watu wawapendao na vitu wanavyovijali zaidi,’’ amesema Mosseri
Mosseri amesema likes na views zitaendelea kuonekana kwa mtumiaji mmoja mmoja katika kipindi hicho cha majaribio lakini hazitaweza kuwekwa wazi kwa watumiaji wengine wa mtandao huo ili kupunguza misuguano na mitazamo hasi inayoweza kusababisha madhara.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanya na Taasisi ya RSPH (Royal Society for Public Health) mwaka 2017 unaeleza kuwa mtandao huo ni hatari zaidi kwa afya ya akili kwa sababu unachangia kupata msongo wa mawazo na mkazoi (depression) na wasiwasi (anxiety).
Wanaoathirika zaidi ni vijana wanaotumia kwa muda mrefu mtandao huo.
We’re currently running a test that hides the total number of likes and video views for some people in the following countries:
✅ Australia
✅ Brazil
✅ Canada
✅ Ireland
✅ Italy
✅ Japan
✅ New Zealand pic.twitter.com/2OdzpIUBka— Instagram (@instagram) July 17, 2019
Latest