Facebook yabuni mfumo mpya wa kupambana na matapeli mtandaoni
- Amebuniwa baada ya kushtakiwa na mwanzilishi wa Money Saving Expert, Martin Lewis.
- Unasaidia kubaini na kudhibiti matangazo yasiyo halisi.
- Unasaidia kuwaepusha watu na wizi mtandaoni unaofanywa na matapeli.
Wiki hii mtandao wa kijamii wa facebook umeanzisha mfumo mpya wa kubaini na kudhibiti matangazo bandia yanayotumia na baadhi ya watu kufanya utapeli mtandaoni.
Mfumo huo mpya unakuja baada ya mtandao huo kushtakiwa Aprili, 2018 na mwazilishii wa tovuti ya matangazo ya Money Saving Expert, Martin Lewis kuhusu picha zake kutumiwa kwenye matangazo bandia yaliyowekwa kwenye mtandao huo wa kijamii.
Martin amesema matangazo hayo yaliharibu heshima yake kwenye jamii lakini mwanzoni mwa mwaka huu aliamua kuachana na kesi hiyo dhidi ya Facebbok kwa masharti mawili.
Zinazohusiana:Facebook kuanza kuwachaguliwa wafuasi wake viongozi wa makundi
Aliitaka Facebook ichangie Paundi milioni 3 sawa na takriban Sh8.6 bilioni kwa ajili ya kuanzisha programu ya kupambana na udanganyifu nchini Uingereza na uazishwaji wa laini ya simu (Citizen Advice Scam Action (CASA)) kwa ajili ya kuwasaidia watu wanapokutana na udanganyifu au utapeli mtandaoni.
Ili kuweza kutumia programu hiyo, utalazimika kwenda upande wa kulia wa mtandao huo wa facebook kwenye kila tangazo ambapo utakutana na alama za nukta itatu ukiponyeza utapata maelezo ya kuripoti tangazo bandia (Misleading or Scam) ambayo yatasaidia Facebook kupitia malalamiko yako na kuyafanyia kazi.
Huenda mfumo huo ukawasaidia watu wengi ambao wamekuwa wakikutana na matapeli au watu wenye nia mbaya ya kujipatia fedha kwa njia isiyo halali kwa kutumia mtandao wa Facebook.