Magufuli awaachia ‘home work’ vigogo wa Tazara

July 25, 2019 12:08 pm · Nuzulack Dausen
Share
Tweet
Copy Link
  • Awataka kupeleka mapendekezo ya namna ya kuboresha reli hiyo yenye uwezo wa kubeba tani zaidi ya milioni tano.

Dar es Salaam. Rais John Magufuli amesafiri kwa treni ya Shirika la reli ya Tanzania na Zambia (Tazara) akielekea Rufiji mkoani Pwani leo huku akiwaachia kibarua vigogo wa shirika hilo kupeleka mapendekezo yatakayosaidia kuboresha usafirishaji wa abiria na mizigo.

Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu iliyotolewa leo imeeleza kuwa Dk Magufuli amesema Serikali inatambua umuhimu wa Tazara na haiwezi kuiacha ikajiendesha kwa ufanisi mdogo usiokuwa na tija kwa Watanzania.

Tazara, moja ya miradi ya kwanza ya China barani Afrika, ina uwezo wa kubeba tani milioni tano kwa mwaka lakini Ikulu imeeleza kuwa kwa sasa inasafirisha tani 300,000 pekee kwa mwaka, kiwango ambacho ni pungufu mara 17 ya uwezo wake.


Tangazo


Mkurugenzi Mkuu wa Tazara Bruno Chingandu na Meneja wa Tazara Tanzania, Fuad Abdallah wamemweleza Rais Magufuli kuwa mapendekezo ya maboresho ya sheria zinazozihusu shirika hilo yameshawasilishwa serikalini ili kuiwezesha kila nchi mbia kuwekeza ili kuboresha usafiri wa abiria na mizigo.

Rais Magufuli, aliyeambatana na mkewe Janet Magufuli katika safari ya kwenda kuzindua mradi wa maporomoko ya maji wa Rufiji, amewaambia vigogo hao kuharakisha mchakato wa maboresho ya sheria hiyo ili kuruhusu ununuzi wa mabehewa na injini za treni ufanyike kwa haraka.

Reli ya Tazara, yenye urefu wa kilomita 1,860, imekuwa ikikabiliwa na changamoto lukuki za kiutendaji jambo lililofanya usafirishaji wake wa mizigo na abiria uwe chini ya kiwango kinachotakiwa kwa mwaka.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
16 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
16 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
16 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Magonjwa haya matano yanayoongoza kwa kuua watu duniani

Magonjwa haya matano yanayoongoza kwa kuua watu duniani

Nukta TV

Mambo yakuzingatia kabla ujawasha gari lako asubuhi

Mambo yakuzingatia kabla ujawasha gari lako asubuhi

Nukta TV

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Nukta TV