Zifahamu filamu za kuangalia siku saba zijazo

August 9, 2019 2:06 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Filamu hizo ni pamoja na ‘Lion King’ iliyoongozwa na John Favreau na ‘Fast and Furious’
  • Zitaonyeshwa katika kumbi mbalimbali za sinema Tanzania kuanzia leo Agosti 9 hadi 15, 2019. 

Dar es SalaamKama wewe ni mpenzi wa filamu na ungependa wiki hii isikupite bila kuburudika kwa angalau filamu moja, basi umepata yote unayoyataka. 

Nukta (www.nukta.co.tz) tumekuletea orodha ya filamu nne ambazo zitaonyeshwa katika kumbi mbalimbali za sinema Tanzania kuanzia leo Agosti 9 hadi 15, 2019. 

Baadhii ya kumbi hizo ni pamoja na Mkuki House, Aura mall, Mlimani City pamoja na Dar Free Market (DFM) jijini Dar es Salaam.

1. Fast and Furious (Hobbs and Shaw)

Filamu hii inawakutanisha Dwayne Johnson (Hobbs), Jason Statham (Shaw) pamoja na Idris Elba (Brixton) ambao wanalazimishwa kuungana japokuwa hawana mawazo sawa ili kupambana na genge la magaidi ili kutengeneza mstakabali mzuri wa maisha yao.

Ikiwa imetumia bajeti ya dola za Marekani mililioni 200 (Sh459.8 bilioni) na kuzinduliwa rasmi Julai 31 mwaka huu, filamu hiyo yenye zuio kwa watazamaji walio chini ya miaka 13 imeongozwa na Muongazaji Filamu, David Leitch ambaye pia ameongoza filamu ya Atomic Blonde na John Wick.

Filamu hii inawakutanisha Dwayne Johnson (Hobbs), Jason Statham (Shaw). Picha|Mtandao.

2. Lion King

Filamu nyingine ambayo haitakiwi ikupite ni ya Lion King ambayo imesheni visa vingi. Baada Mfalme Mufasa kuuwawa na mdogo wake (Scar), mtoto wake Simba (Donald Glover) anabaki njia panda na hajui kama yupo tayari kupokea majukumu kama mfalme. Je Nala (Beyonce) ataweza kumshawishi Simba kurudia nafasi yake? 

Fuatilia filamu hiyo iliyogharimu Dola za Marekani milioni 260 (Sh597.7) chini ya kiongozi John Favreau kichwa nyuma ya filamu ya Avengers Engame  iliyotoka mwaka huu wa 2019 na Jungle Book ya 2016.


Zinazohusiana


3. Angry Birds

Filamu hii inaelezea kisiwa kilichojaa ndege wenye furaha na amani kinapata ugeni wa nguruwe lakini unajua kilichotokea baada ya kupata ugeni huo? Basi wiki hii utapata mkasa mzima wa filamu hiyo. Filamu hii ina lengo kuwafunza watoto juu ya ushirikiano na umuhimu wa kuwa na marafiki.

Hiyo ni kazi ya Red (Jason Sudeikis), Chuck (Josh Gad) na Bomb (Danny McBride) ambao watakuinyesha lengo la nguruwe hao kuingia katika kisiwa hicho kutokana na umahiri wa Muandaaji wa filamu hiyo Clay Kaytis ambaye ameongoza filamu za vibonzo (Animation) ikiwemo ya Tarzan na Mulan. 

4. Spider Man (Far from Home)

Ikiwa ni filamu ya 23 kwenye ulimwengu wa sinema wa kampuni ya Marvel (MCU), ‘Far from Home’  imeongozwa na Kelvin Feige ambaye ni Rais wa kampuni ya Marvel tangu 2007, pia yupo nyuma ya filamu ya Captain Marvel pamoja na Avengers Infinity War. 

Nini kitamkuta Peter Parker (Tom Holland) katika kupambana na Furry (Samuel Jackson) Ikizingatiwa kuwa hawezi kudhibiti nguvu zake kama awali katika filamu hiyo iliyogharimu Dola za Marekani milioni 160 (Sh367.8 bilioni) kuitengeneza na ambayo hairuhusu kuangaliwa na watoto wenye umri chini ya miaka 13?.

Kuangalia filamu hizi, fika kwenye maduka makubwa (malls) kuanzia saa sita mchana na kuendelea Agosti 9 hadi 15, 2019. 

Filamu ya Spider Man (Far from Home) nayo wiki hii itaonyeshwa katika kumbi mbalimbali Tanznaia. Picha|Mtandao.

Enable Notifications OK No thanks