Maswali lukuki mfumo mpya wa Harmony OS, Huawei

August 15, 2019 10:29 am · TULINAGWE ALSON
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni mfumo mpya endeshi unaotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni na kampuni ya simu Huawei.
  • Imeleta maswali mengi kwa wataalamu wa kuunda mifumo ya kompyuta na simu juu ya utendaji kazi wake.
  • Huawei imeamua kuanzisha jukwaa baina yake na wataalamu wa programu ili kuendeleza mfumo huo.

Dar es Salaam. Takriban miezi mitatu tangu ya Marekani ya Google itangaze kusitisha huduma ya mfumo endeshi wa Android kwa vifaa inavyotengenezwa na Huawei, kampuni hiyo ya China imeamua kutengeneza mfumo wake mpya uitwao Harmony OS. 

Uamuzi wa Google kusitisha huduma za Android kwa Huawei, licha ya kuwa mdau wake mkubwa wa kibiashara, ulikuja baada ya Serikali ya Marekani kuiweka kampuni hiyo ya China katika orodha ya kampuni zisizotakiwa nchini humo kutokana na matatizo ya kiusalama. 

Hata hivyo, Harmony OS inatarajiwa kuwa ni mbadala wa Android, iliyozoeleka na watumiaji wa vifaa hivyo vya Huawei. 

Huawei, ambayo ni kampuni ya pili duniani kwa uzalishaji wa simu janja nyuma ya Samsung, ilitangaza mfumo huo kwa kushtukiza mapema wiki iliyopita katika mkutano nchini China na kumaliza fununu za ujio wa injini ya kuendeshea vifaa vyake vya kielektroniki hususan simu janja na tabiti. 

Kwa kuanza, Huawei imeeleza kuwa Harmony OS itaanza  kutumika katika vifaa kama saa za kielektroniki (smart watches), spika na televisheni za kisasa huku simu zikitarajiwa kuanza kutumia mfumo huo miaka mitano ijayo baada ya kutengamaa au kusitishwa kwa mfumo wa Android kwenye simu.

Wakati Huawei ikiendelea kuimarisha mfumo wake huo mpya, bado kumekuwa na wasiwasi mkubwa miongoni mwa watumiaji wa simu za kampuni hiyo na wataalamu wa programu za simu na kompyuta juu ya ufanisi wake.

Wasiwasi huo unatokana na kuwepo kwa maswali lukuki ambayo hadi sasa Huawei bado hawajafikia hatua ya kuyajibu likiwemo iwapo Harmony OS itakuwa rafiki zaidi kwa watumiaji wake kama ilivyo kwa Android. 


Soma zaidi: 


Hofu nyingine kubwa iliyopo kwa wamiliki wa kampuni hiyo ni kupata wataalamu wa programu (developers) kwa ajili ya kutengeneza programu tumishi (applications) zitakazoweza kufanya kazi kwa ufanisi ndani ya mfumo huo katika vifaa mbalimbali vya kielektroniki vya Huawei.

Changamoto hiyo ya upatikanaji wa watengeneza programu hao imeanza kutengeneza hofu iwapo mfumo huo utawafikia watu wengi kama ilivyo kwa mifumo mingine maarufu ya Android na iOS inayomilikiwa na kampuni ya Apple ya Marekani.

Mfumo wezeshi kwajili ya kampuni ya Huawei. Picha na Mtandao.

Baadhi ya watumiaji wa simu hizo na watengeneza programu wamesema bado kuna maswali lukuki yanayotakiwa kujibiwa ili kupata picha kamili juu ya namna mfumo huo utakavyofanya kazi na kurahisisha mawasiliano. 

Miongoni mwa maswali hayo ni, je, mfumo Harmony Os itakuwa na uwezo wa kuboreshwa kama mifumo mingine na kuongeza ufanisi katika vifaa hivyo?  Je, mfumo huo utaweza kuzoeleka haraka na watumiaji kama ilivyokuwa kwa Android? Watengenezaji wa programu watakuwa huru kutengeneza programu tumishi kupitia mfumo huo kama ilivyo kwa Android?

Baadhi ya watengenezaji wa programu wameaimbia Nukta (www.nukta.co.tz) kuwa iwapo mfumo huo utakuwa na vigezo kama Android utakuwa umekidhi matarajio yao katika utengenezaji wa ‘applications’ za kuuzia wateja baada ya uzinduzi rasmi wa mfumo huo. 

“Mfumo huo ukiwa rafiki kwetu kwajili ya kutengeneza applications na kuboresha baadhi ya vitu katika mfumo huo itakua vizuri zaidi kwani inatusaidia na sisi kuridhisha wateja wetu,” amesema mtaalamu mmoja wa programu za kompyuta na simu wa jijini Dar es Salaam. 

Ili kujenga uhusiano mzuri baina ya wabunifu na wamiliki wa kampuni hiyo, Huawei imeandaa jukwaa litakalohusisha wabunifu na wahusika uitwao Huawei OS (Open Source Foundation) utakaokua na lengo kuu la kudumisha ushirikiano kati ya kampuni na wabunifu mbalimbali.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW