Google, Expedia wazindua bidhaa mpya ya safari

October 12, 2019 5:18 am · TULINAGWE ALSON
Share
Tweet
Copy Link
  • Wamezindua teknolojia  itakayomwezesha msafiri kuratibu safari na mahali atakapofikia kwa njia rahisi ya kinasa sauti.
  • Baadhi ya watu waifagilia wasema inawasaidia kufika popote duniani.

Kampuni za Google na Expedia wamerahisisha mchakato wa kusafiri kimataifa kwa ajili ya shughuli mbalimbali ikiwemo mapumziko ya mwisho wa mwaka.

Expedia Action, kampuni inayoratibu usafiri wa ndege ikishirikiana na moja ya bidhaa ya Google ya “Google Assistant” wamezindua teknolojia  itakayomwezesha msafiri kuratibu safari na mahali atakapofikia kwa njia rahisi ya kinasa sauti.

Mtu anayetaka kutumia teknolojia hiyo anapaswa kufungua akaunti katika aprogramu tumishi ya Google Assistant kisha na ataunganishwa na mfumo wa expedia ili kupata urahisi anapotoa taarifa zake kabla hajaanza safari.

Programu hii inawafaa zaidi wale wanaosafiri nchi za nje ambazo hawana uzoefu nazo, kwani inamsaidia kupata usafiri wa uhakika na mahala pazuri pa kufikia ikiwemo hoteli inayoendana na mfuko wake. 

Pia inampa mtu taarifa za kina za eneo analokwenda na kumshauri ni vitu gani anapaswa kubeba ili kuendana na mazingira mapya atakayofikia.


Zinazohusiana:


Nancy George mtalii kutoka Tanzania anayetarajia kusafiri hivi karibuni  kuelekea Uingereza kwa mara ya kwanza ameiambia www.nukta.co.tz  kuwa teknolijia hiyo itamrahisishia safari yake na kuifanya iwe ya mafanikio, kwa sababu teknolojia hiyo inatoa suluhisho kamili.

“Moja ya mambo yaliyokuwa yananitatiza ni mazingira nitakayoenda kukutana nayo, ambapo sitakua najua kitiu chochote,” amesema Nancy na kueleza kuwa baada ya kuifahamu teknolojia hiyo, sasa hana wasiwasi tena.

Teknolojia hiyo ni muendelezo wa wabunifu kubuni programu rahisi zinazoweza kuwawezesha wasafiri kwenda mahali popote bila kuhofia usalama wao, kwa sababu inawaongoza kwa kila kitu wanachofanya.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
13 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
13 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
13 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

Nukta TV

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Nukta TV

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Nukta TV