Twitter yaanika sera ya matangazo ya kisiasa kwenye mtandao wake

November 20, 2019 4:52 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Katazo hilo litanza kuanzia  Novemba 22
  • Halitavikumba vyombo vya habari vilivyofikia vigezo vilivyowekwa

Dar es Salaam. Ikiwa ni siku chache kuelekea Novemba 22, 2019 ambapo mtandao wa twitter utasimamisha matangazo ya kisiasa, uongozi wa mtandao huo umetoa sera ambazo zinazungumzia mustakabadhi mzima wa hatua hiyo.

Kitendo cha mtandao huo kutoruhusu matangazo ya kisiasa kimekuja na lengo la kuwafanya  wanasiasa kufanya kazi ili kwa kutumia ushawishi wao na siyo kununua ushawishi kwa njia ya matangazo ambayo yalikuwa yakiruhusiwa kwenye mandao huo.

Taarifa iliyotolewa na twiter inasema siyo kwamba hakutakuwepo na matagazo yoyote yanayohusisha siasa bali, ni wanasiasa hawataweza kutumia mtandao huo kwaajili ya kushawishi ama kushinikiza wananchi kuenenda na siasa zao.​

Vyombo vya habari vitaruhusiwa kuweka maudhui yakisiasa ambayo huenda yakawa habari na taarifa muhimu. Picha| Mtandao.

Aidha, matangazo ya siasa ambayo yataruhusiwa ni yale ambayo yanatoka kwenye vyombo vya habari ambavyo vinakidhi vigezo vya kufanya matangazo kwenye twitter.

Vyombo vya habari vitaruhusiwa kuweka maudhui yakisiasa ambayo huenda yakawa habari na taarifa muhimu lakini pia hii siyo kwa kila chombo cha habari bali vile ambavyo vimekidhi vigezo vilivyotolewa na twitter.

Maudhui yanayoruhusiwa kwenye vyombo vya habari siyo ya kukinzana au kukubaliana na chama au mwanansiasa yeyote.


Zinazohusiana

Sababu za Twitter kusitisha matangazo ya kisiasa Novemba 22


Matangazo ya kisiasa ni yapi?

Kwa mujibu wa mtandao wa twitter, matangazo ya kisiasa ni yale ambayo yanamlenga moja kwa moja mgombea wa kisiasa, chama cha kisiasa, kura za maoni, kura, taratibu za kisiasa, matokeo ya kimahakama, sheria na maelekezo ya kisiasa.

Pia ni matangazo yoyote ambayo yanahusisha rufaa za kura, maombi ya misaada ya kifedha na utetezi wa jambo lolote lilitojwa.

“Haturuhusu matangazo ya aina yeyote kutoka kwa wagombea, vyama vya kisiasa au watumishi wa serikali walioteuliwa au kuchaguliwa,”  imeandika sehemu ya sera hiyo  ya twitter.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW