Kijue kitufe wanachokikwepa wapishi wakati wa kutumia “Microwave”

November 29, 2019 12:04 pm · TULINAGWE ALSON
Share
Tweet
Copy Link

Wapishi wanakikwepa kwa sababu mara nyingi hakileti matokeo yaliyokusudiwa. Picha | Mtandao.


  • Kitufe kinaitwa “Defrost Button”, kinatumika kuyeyusha chakula kilichoganda au kibichi.
  • Wapishi wanakikwepa kwa sababu mara nyingi hakileti matokeo yaliyokusudiwa.
  • Washauriwa kutumia njia za kawaida kupashia kwenye mashine hiyo.

Huenda ukawa mmoja ya watu wanaopenda kupasha au kuandaa chakula kwa kutumia mashine ya kupashia chakula (Microwave). Na inaweza ikawa moja ya mashine zisizikosekana katika nyumba yako kwa sababu ni njia rahisi ya kupasha chakula wakati wowote.

Lakini kuna utaalamu wa kutumia mashine hizo. Kwa mujibu wa mtandao wa Reader’s Digest, kitufe kiitwacho “Defrost Button” kwenye mashine hizo ambacho hakitumiwi sana na watu wenye mashine hizo.

“Defrost Button” ni kitufe kinachotumika kuyeyusha chakula kilichoganda au kuandaa chakula chenye ubichi katika mashine za kupashia chakula.

Baadhi ya wataalam wa mapishi  wameongelea ni kwa namna gani kitufe hicho hakitumiki na kina matumizi machache kwa watu wengi. 

Imelda Gerald mtaalam wa mapishi katika hoteli ya Hyatt Regency ya jijini Dar es Salaam, amesema kitufe hicho hakitumiki kwa sababu ya matokeo ya uaandaaji wa chakula ni madogo na wakati mwingine ufanisi siyo mzuri sana.

“Kwa matumizi ya kitufe hicho, kwa asilimia kubwa hatupendi kukitumia kwa sababu kina uwezo wakubakisha barafu kwenye chakula kilichokuwa kimeganda na kwa asilimia kubwa hakileti matokeo chanya kwenye uandaaji wa chakula chako,” amesema Imelda.


Soma zaidi: Ukweli kuhusu athari vyombo vya plastiki vinavyotumika kupashia chakula kwenye “Microwave”


Hata hivyo, kwa watumiaji wa mashine hizo za kupashia chakula, hushauriwa kutumia njia ya kawaida ya kupashia chakula na kwa chakula kilichoganda ni vyema kusubiri kiyeyuke kwanza kabla ya kuingiza kwenye Microwave.

mia kitufye hicho ni kwamba hakifanyi maandalizi mazuri ya chakula kiasi kwamba kinaweza kusababisha ubichi kupaki kwenye chakula au kutokupasha vizuri chakula licha ya spidi iliyopo katika kupasha.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
17 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
17 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
17 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Msemaji Geita: Vijana msikurupuke kuja Katoro

Msemaji Geita: Vijana msikurupuke kuja Katoro

Nukta TV

Magonjwa haya matano yanayoongoza kwa kuua watu duniani

Magonjwa haya matano yanayoongoza kwa kuua watu duniani

Nukta TV

Mambo yakuzingatia kabla ujawasha gari lako asubuhi

Mambo yakuzingatia kabla ujawasha gari lako asubuhi

Nukta TV