Dhahabu yachangia kupaa thamani ya bidhaa, huduma nje ya nchi Oktoba

December 18, 2019 7:14 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Thamani ya mauzo ya bidhaa na huduma za Tanzania zilizosafirishwa nje ya nchi kwa mwaka unaoishia Oktoba 2019 imeongezeka kwa asilimia 10.3.
  • Imechagizwa zaidi na dhahabu iliyochukua asilimia 39.3 ya thamani ya bidhaa zilizosafirishwa nje ya nchi. 
  • Thamani ya bidhaa za asili imeshuka isipokuwa chai na kahawa. 

Dar es Salaam. Thamani ya mauzo ya bidhaa na huduma za Tanzania zilizosafirishwa nje ya nchi kwa mwaka unaoishia Oktoba 2019 imeongezeka kwa asilimia 10.3 ikichagizwa zaidi na bidhaa zisizo za asili ikiwemo dhahabu.

Ripoti ya Mapitio ya mwezi ya Uchumi (Monthly Economic Review) iliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inaonyesha kuwa thamani ya mauzo ya bidhaa na huduma zilizosafirishwa nje ya nchi iliongezeka hadi kufikia dola za Marekani 9,472.3 milioni sawa na Sh21.7 trilioni kutoka dola 8,742 milioni (Sh20.1 trilioni) katika kipindi kama hicho mwaka jana.

Ongezeko la thamani ya mauzo hayo lilichagizwa zaidi na mauzo ya bidhaa zisizo za asili hasa madini ya dhahabu ambayo yalichukua asilimia 50.4 ya mauzo yote ya bidhaa zisizo za asili na asilimia 39.3 ya bidhaa zote zilizosafirishwa nje ya nchi katika kipindi hicho.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa kuimarika kwa mauzo ya dhahabu nje ya nchi, kumechangiwa na hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuimarisha operesheni za kusimamia shughuli za uchimbaji madini nchini.

“Sambamba na hilo, thamani ya bidhaa za viwandani zilizosafirishwa nje ya nchi ziliongezeka kwa asilimia 41 hadi dola za Marekani 1,068.1 milioni (Sh2.5 trilioni) ikichagizwa na bidhaa za chuma, vioo na vyombo vya vioo, tumbaku ya viwandani na mbolea,” inaeleza sehemu ya ripoti hiyo. 


Zinazohusiana: 


Huduma nyingine zilizochangia kuongezeka kwa thamani ya mauzo nje ya nchi ni pamoja na huduma zinazotolewa katika sekta ya utalii, usafirishaji, ujenzi, bima, fedha, habari na mawasiliano.

Hata hivyo, thamani ya bidhaa zote za asili zilizosafirishwa katika mwaka unaoishia Oktoba 2019 imepungua kwa asilimia 40.5 hadi dola za Marekani 688.7 milioni (takriban Sh1.5 trilioni), isipokuwa mazao ya chai na kahawa. 

“Kuongezeka kwa thamani ya kahawa na chai iliyosafirishwa kwa kiwango kikubwa ilichangiwa na hali ya hewa nzuri katika kipindi cha uzalishaji wa mazao hayo,” inaeleza ripoti hiyo.

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Nukta TV

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Nukta TV

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Nukta TV